Sports
Sane Sasa Ni Mali Ya Galatasaray

Ni rasmi aliyekua kiungo wa Manchester cityna Bayern Munich ya Ujerumani Leroy Sane amekamilisha uhamisho wake katika kilabu ya Galatasaray ya Uturuki bila ada yoyote.
Sane mwenye umri wa miaka 30 amepasi vipimo vya kimatibabu baada ya kuwasili mjini Istanbul alipolakiwa na mshabiki wengi wa kilabu hiyo anapojiunga na mabingwa hao wa ligi ya Uturuki.
Mchezaji huyo alijiunga na Bayern Munich msimu wa mwaka 2020 akitokea Mancity kwa mkataba wa miaka mitano na amefanikiwa kufunga magoli 61 katika mechi 220 ambazo amechezea timu hio.
Kiungo huyo pia amekua nguzo muhimu kwa timu ya taifa la Ujerumani akifanikiwa kufunga magoli 14 katika mechi 70 ambazo ameshirikisha katika timu hiyo.
Sane ni miongoni mwa wachezaji walionyeshwa mlango na kilabu ya Bayern Munich kwa msimu mpya.
Sports
Florian Wirtz Sasa Mambo Nywee! Kutua Liverpool

Kilabu ya Liverpool imeafikia makubaliano na Bayern Leverkusen kuhusiana na usajili wa kiungo mbunifu Florian Wirtz uhamisho ambao ni rekodi mpya wa uhamisho Uingereza.
Timu hizo mbili zimekua kwenye mazungumzo na sasa kitita cha pauni milioni 116 imeafikiwa kwa tineja huyo mwenye umri wa miaka 22.
Raia huyo Ujerumani sasa atawasili Liverpool kwa ajili ya vipimo vya kimatibabu wiki ijayo na baadaye kutiwa wino kandarasi mpya
Inaaminika Wirtz atamwaga wino mkataba wa miaka mitano na The Reds na kuwa sajili wa pili kwa kocha Arne Slot baada ya kupata sahihi ya beki Jeremie Frimpong wa taifa la Uholanzi kwa pauni milioni 29.5.
Sports
Thomas Frank Kocha Mpya Spurs

Kilabu ya Tottenham HotSpurs ya Uingereza imemtambulisha Thomas Frank kuwa kocha mpya kumrithi Ange Postecoglou aliyepigwa kalamu mwezi jana licha kushinda kombe la Europa ligi na kilabu hiyo wakishinda Manchester United goli 1-0.
Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 51 amemwaga wino kwenye karatasi mktaba wa miaka mitatu na kilabu hiyo ya London Kaskazini huku kibarua cha kwanza ni kutoa kilabu hiyo kutoka nafasi ya 17 Epl na kurejesha katika ubora wake.
Raia huyo wa Denmark amekua na kilabu ya Brenford kwa miaka saba na aliwasaidia The bees kumaliza ya kumi msimu jana na alama 56 ligi ya Epl na amekua akiwindwa ni vilabu kadha wa kadha.