Connect with us

Business

Redio Zapoteza Soko Kilifi, Wafanyabiashara Wabadilika Kuuza Nguo

Published

on

Ujio wa tekinolojia umetajwa kuathiri biashara ya kuuza radio mjini kilifi kaunti ya kilifi.

Kulingana na wafanyibiashara wa kuuza radio mjini kilifi biashara hiyo imedorora pakubwa kwani simu nyingi za mkononi ziko na radio.

Wakizungumza na cocofm wafanyibiashara hao wamesema kuwa mara kwa mara wamekosa kuuza kutokana na idadi ndogo ya wateja hali ambayo imeathiri mapato yao.

Hata hivyo wafanyibiashara hao wamesema imewalazimu kuanzisha biashara ya kuuza nguo ili kuendelea kujikimu kimaisha.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Business

Kanisa Katoliki lahimiza umuhimu wa Kilimo

Published

on

By

Kasisi wa Kanisa Katoliki jimbo la Malindi Misheni ya Mere kaunti ya Kilifi, Blaise Kamau Andrew ametoa wito kwa wenyeji wa Pwani kuwekeza zaidi katika kilimo cha kisasa ili kupata chakula cha kutosha na kilicho bora.

Akizungumza katika eneo la Kwa Ndomo eneo bunge la Malindi, Kasisi Kamau aliesema ikiwa Wapwani watatia juhudi katika sekta ya kilimo huenda kukawa na mavuno mengi na chakula cha kutosha ili kudhibiti njaa wakati wa kiangazi.

Kasisi Kamau pia aliwashinikiza kuchimba visima vingi vya maji ili panapokosekana mvua kuwe na maji ya kutosha ya kuendeleza kilimo nyunyizi.

“Chibeni visima ili usiwe mkulima wa kungojea tu mvua ya mwenyeji Mungu.Tufanyeni bidi wengi wenu wana Ng’ombe, wengi wenu wana mbuzi uza Ng’ombe mbili, chimba kisima maji hayako mbali sana ili mvua ikikatika bado mnaendeleza kilimo nyunyizi’’, alisema Kasisi Kamau.

Ni kauli ambayo imeungwa mkono na msimamizi wa kitengo cha chakula na Kilimo katika benki ya Equity tawi la Nairobi, George Macharia ambaye alisema ili kuimarisha uchumi wa Kenya ni lazima Wapwani na wakenya kwa jumla wakumbatie kilimo cha kisasa kupitia mfumo wa teknolojia.

“Ili tuweze kupanua uchumi ni lazima tuwekeze katika kilimo na tuhakikishe tunatumia kilimo cha kisasa cha kiteknolojia’’, Macharia aliwasihi Wakulima.

Taarifa ya Janet Mumbi

Continue Reading

Business

Kanda ya Pwani kuimarika kupitia Kilimo cha kisasa

Published

on

By

Kanda ya Pwani inatarajiwa kuimarika zaidi kupitia Kilimo cha kisasa kinachotekelezwa kupitia mfumo wa teknolojia.

Hii ni kupitia mikakati inayoendelezwa na Agitech Seedlings kuhakikisha Wakulima na Wenyeji wa Kanda ya Pwani wanakumbatia Kilimo cha kisasa kama maeneo mengine nchini.

Akizungumza na Coco FM katika maonyesho ya Kilimo cha kisasa na uzinduzi wa tawi jipya la Agitech Seedling katika eneo la Kwa Ndomo mjini Malindi kaunti ya Kilifi, Mkurugenzi wa Agitech Seedlings Peter Karanja Ndung’u alieleza sababu za kuanzisha Kilimo hicho cha kisasa katika ukanda wa Pwani.

Karanja pia alisema wanapania kuhakikisha wenyeji wa Pwani wanahamasishwa ipasavyo na hata kuonyeshwa namna ya kufanya Kilimo hicho hapa pwani.

“Kupitia hamasa ambazo tunatoa kwa wakulima na wenyeji wa Pwani kwa jumla tunatarajia kuwa Kilimo kitaanza kuimarika na kuondoa dhana ambayo imekuwepo kwamba eneo la Pwani linatambulika pekee kwa masuala ya uvuvi’’, alisema Karanja.

Vilevile, Karanja alisema kuna haja ya Wakulima kutunza ardhi zao kwa kuhakikisha zina rutuba ya kutosha ili kuzalisha chakula kwa wingi na bora.

Taarifa ya Janet Mumbi

Continue Reading

Trending