Connect with us

News

Oscar Wanje Awakashifu Wawakilishi Wadi Wenza

Published

on

Mwakilishi wadi wa Ganda, kaunti ndogo ya Malindi, kaunti ya Kilifi, Oscar Wanje amekemea vikali tukio ambapo wawakilishi wadi wawili walihusika katika mshikemshike wa kumpiga mwakilishi wadi maalum, Elina Mapenzi, baada ya kutofautiana bungeni.

Akizungumza kupitia mtandao wake wa kijamii, Wanje amesema kuwa kitendo hicho kilidhihirisha utovu wa nidhamu lakini pia dhulma dhidi ya wanawake ikizingatiwa kwamba wawakilishi wadi hao waliompiga Mapenzi walikuwa wa kiume.

Wanje amekitaja kitendo hicho kama ukiukaji wa demokrasia kwani kuna uhuru wa viongozi kutofautiana katika maswala mbalimbali.

Ni mvutano ambao ulimpelekea Mapenzi kupata majeraha.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Godhana, awataka wakaazi kutoingiza siasa miradi ya maendeleo

Published

on

By

Gavana wa kaunti ya Tana River Dhadho Godhana amewataka wenyeji wa kaunti hiyo kujiepusha na wanasiasa ambao wanaingiza siasa kwenye masuala ya maendeleo.

Godhana alisema hilo limechangia kaunti ya Tana River kusalia nyuma kimaendeleo hali ambayo itasababisha miradi mingi kuzidi kukwama.

Godhana alisema ni lazima viongozi na wenyeji wa kaunti ya Tana River washirikiane na uongozi wa kaunti ili kuafikia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Wakati huo huo Godhana aliesema mradi wa Village Cluster ambao umekuwa ukipingwa ndio utakaosaidia kudhibiti changamoto ambazo zinaikumba kaunti ya Tana River.

Naye Mahat Ali Loka ambaye ni Naibu Gavana wa kaunti ya Tana River, aliwaonya wanasiasa kutoka kaunti zingine dhidi ya kuingilia siasa za kaunti hiyo huku Spika wa bunge la kaunti hiyo Osman Noor Galole, akitoa onyo kwa wafanyikazi wa umma dhidi ya kujumu la serikali ya kaunti ya Tana River.

Taarifa ya Janet Mumbi

Continue Reading

News

Mwili wapatikana baharini Shelly Beach Likoni

Published

on

By

Polisi kaunti ya Mombasa wanachunguza kisa ambapo mwili wa mwanamme ambaye hajafahamika umepatikana ukielea katika maji ya bahari hindi kwenye ufuo wa Shelly Beach eneo bunge la Likoni.

Ripoti ya polisi ilibaini kuwa mwili huo uligunduliwa na wavuvi eneo hilo, ambao walipiga ripoti katika kituo cha polisi cha Shelly Beach kuhusiana na tukio hilo.

Polisi walisema hawakubaini mara moja anakotoka mtu huyo.

Vile vile haikubainika iwapo marehemu alizama au aliuawa kabla ya mwili wake kutupwa baharini.

Polisi walisema hawajakutana na stakabadhi zozote za kumtambulisha mtu huyo huku wakiwasihi wananchi kutoa taarifa iwapo wanafahamu familia ya marehemu.

Mwili unahifadhiwa katika hifadhi ya maiti katika hospitali ya Rufaa ya Coast General Mombasa wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading

Trending