Sports
Nairobi United Ndio Mabingwa FKF Cup

Kilabu ya Nairobi United ndiyo mabingwa wa kombe la FKF Cup baada ya kunyuka Gor Mahia magoli 2-1 uwanjani Ulinzi Sports Complex hapo jana.
Kiungo Frank Ouya aliwatanguliza Nairobi United dakika ya 6 kabila ya Ben Stanley Omondi kuchomolea Kogalo dakika ya 37.
Goli la ushindi la Nairobi United lilitiwa kambani na Enock Machaka dakika ya 73 kipindi cha pili. United sasa ambao wanaingia FKF PL kwa mara ya kwanza itawakilisha Kenya kwenye taji la Mashirikisho Afrika CAF Confederation.
Katika mechi ya kusaka nafasi ya Tatu Muranga Seal 1-0 Mara Sugar.
Continue Reading
Sports
Manchester United Ndiyo mabingwa wa ‘PREMIERE LEAGUE SUMMER SERIES’

Manchester United imetwaa ubingwa wa kombe la ‘Premier League Summer Series’ kufuatia sare ya 2-2 dhidi ya Everton katika dimba la Mercedes-Benz, Atlanta, Georgia Marekani.
Michuano hiyo ya maandalizi ya msimu mpya ilishirikisha timu nne za Ligi Kuu England Man United, West Ham United, Everton na Bournemouth ambapo Mashetani hao Wekundu wamemaliza kileleni pointi 7 baada ya mechi tatu, wakishinda mechi mbili na kutoka sare mechi moja.
Kiungo Bruno Fernandes aliwaweka uongozini United dakika ya 18 kupitia mkwaju wa Penalti au Tuta kisha Iliman Ndiaye akisawazishia The Toffees dakika ya 40,United tena walichukua uongozi kupitia kwa kiungo mshambulizi Mason Mount dakika ya 69 kabila ya beki Ayden Heaven kujifunga dakika ya 75.
MSIMAMO:
1. Man UTD — mechi 3 — pointi 7
2. West Ham mechi 3 — pointi 6
3. Bournemouth mechi 3 — pointi 3
4. Everton mechi 3 — pointi 1
Sports
Stars yaanza vema CHAN kwa ushindi goli 1-0 dhidi ya DR-Congo

Timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars) imechukua alama zote tatu kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi B wa kombe la Mataifa Afrika CHAN 2024 katika dimba la Moi Sports Centre, Nairobi.
Goli hilo la kipekee lilitiwa wavuni na kiungo mshambulizi Austine Odhiambo dakika 45 kipindi cha kwanza.
Rais William Ruto ambaye alifuatilia mechi hiyo uwanjani alitembelea kikosi katika chumba cha kubadilisha na kukabidhi ahadi yake ya shilindi milioni moja kwa kila mchezaji baada ya ushindi huo.
Stars wamekwea kileleni mwa kundi A na alama Tatu kundi ambalo pia lina Morocco,Zambia na Angola Mechi ijayo ya Stars ni dhidi ya Angola ni Agosti 7.