Connect with us

Sports

Morocco Waanza Mazoezi Nyayo Tayari Kwa CHAN

Published

on

SIKU 4 ZIMESALIA KUNGOA NANGA KOMBE LA CHAN
Timu ya Taifa Ya Morocco marufu ‘Atlas Lions ‘ wamefanya mazoezi Yao ya kwanza Ugani Nyayo hapo jana kujinoa tayari kwa mechi ya ufunguzi.
Vijana hao waliwasili mapema Jana tayari kwa kipute hicho kinachongoa nanga Jumamosi hii ugani Benjamin Mkapa nchini Tanzania.
Badhi ya wachezaji nyota kwenye kikosi hicho ni pamoja na;mshambulizi El Mahraoui Anas pamoja na kiungo Khairi Ayoub wa RS Berkane.
Hii hapa ni kikosi chote cha Taifa hilo kwa kombe la CHAN;
Magolikipa:
  • Al Harrar Elmehdi
  • Rachid Ghanimi (FUS Rabat)
  • Aqzdaou Omar (Wydad Casablanca)

Mabeki:

  • Moufid Mohamed (Wydad Casablanca)
  • Boulacsout Mohamed
  • Mchakhchekh Mehdi
  • Louadni Marouane
  • Arrassi Bouchaib
  • Assal Abdelhak (RS Berkane)
  • Belammari Youssef (Raja Casablanca)
  • Zahouani Fouad

Viungo:

  • Khairi Ayoub (RS Berkane)
  • Hrimat Mohamed Rabie
  • Souane Amine
  • Essadak Houssam
  • Hajji Reda (RS Berkane)
  • Bach Anas
  • Aït Ouarkhane Khalid
  • Bougrine Sabir

Washambulizi:

  • Mehri Youssef (RS Berkane)
  • El Mahraoui Anass
  • Bouhra Saïf-Eddine (Wydad Casablanca)
  • Baba Khalid
  • Riahi Imad (RS Berkane)
  • Salaheddine Errahouli
  • Mouloua Ayoub
  • El Kaabi Youness
  • Lamlioui Oussama (RS Berkane) Morocco wanafungua kampeini Yao dhidi ya Angola siku ya Jumapili Ugani Nyayo kwenye kundi A.
Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Sports

Winga Wa Colombia Luis Diaz Sasa Ni Mali Ya Bayern

Published

on

By

Klabu ya Bayern Munich, inayoshiriki Ligi Kuu ya Bundesliga nchini Ujerumani, imetangaza kumsajili winga wa Colombia, Luis Díaz.

Hatua hii imekuja baada ya Bayern Munich na Liverpool kufikia makubaliano kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo kwa ada ya pauni milioni 65.5.

Díaz, mwenye umri wa miaka 28, aliwasili mjini Munich hapo jana kwa ajili ya vipimo vya kitabibu kabla ya kutia saini mkataba wa miaka minne na mabingwa hao wa Ujerumani.

Mchezaji huyo alijiunga na Liverpool mwaka 2022 akitokea klabu ya Porto kwa ada ya pauni milioni 37. Tangu wakati huo, ameifungia Liverpool mabao 41 katika mechi 142 alizocheza uwanjani Anfield.

Nyota huyo aliondoka kwenye kambi ya mazoezi ya Liverpool mjini Hong Kong hapo jana na kujiunga rasmi na waajiri wake wapya kwa maandalizi ya msimu mpya.

Continue Reading

Sports

Timu Ya Taifa Ya Nigeria Super Falcons Imepokea Zawadi Nono Kutoka Kwa Rais

Published

on

By

 Mabingwa wa Bara Afrika kwa soka la akina dada Super Falcons wamevuna vinono kutoka kwa rais wa taifa hilo punde tu baada ya kutua kutoka mjini Rabat Morocco.
Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu akitangaza zawadi zifuatazo kwa timu ya Super Falcons:
Kila mchezaji atapokea dola 100,000 za Kimarekani
Kila mchezaji atapewa nyumba ya vyumba vitatu
Kila mwanachama wa benchi la ufundi atapokea dola 50,000 za Kimarekani
Zaidi ya hayo, Jukwaa la Magavana wa Nigeria limewazawadia kila mchezaji kiasi cha ₦10 milioni (takriban dola 6,000 za Kimarekani).
Vipusa hao waliwashinda wenzao wa Morocco magoli 3-2 kwenye fainali kali iliosakatwa siku ya Jumamosi na kutwa ubingwa huo likiwa ni taji lao la kumi katika historia ya kombe hilo.
Continue Reading

Trending