Connect with us

Business

Mombasa Yapoteza Watalii kwa Zanzibar, Waziri Ataka Mageuzi

Published

on

Waziri wa Utalii, Utamaduni na Biashara katika Kaunti ya Mombasa, Mohammad Osman, amesema sekta ya utalii imekuwa ikidorora katika miaka ya hivi karibuni, hali ambayo huenda ikaathiri uchumi wa kaunti hiyo.

Akizungumza na wanahabari, jijini Mombasa waziri Osman ameitaka serikali kufungua anga za Kenya kuwa huru kwa mashirika ya ndege ya kimataifa, ili kuongeza idadi ya watalii wanaowasili humu nchini .

Kwa mujibu wa waziri huyo, kwa muda mrefu Mombasa imekuwa ikishindana na Zanzibar kama kivutio kikuu cha watalii Afrika Mashariki, ila mwaka jana Zanzibar ilipokea zaidi ya watalii 800,000 huku Mombasa ikipokea takribani 200,000 pekee.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Business

Mradi wa kiuchumi wa Dongo Kundu wavutia wawekezaji zaidi

Published

on

By

Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wanaendelea kuonyesha nia ya kuekeza katika mradi wa kiuchumi wa dongo kundu kaunti ya Mombasa.

Mradi huo unaotarajiwa kuongeza uzalishaji katika viwanda na thamani ya bidhaa ndani ya nchi na nje, unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Kampuni ya nishati kutoka China, Ruike Energy Group Limited, ni mwekezaji wa hivi karibuni kuonyesha nia ya kupata nafasi ndani ya eneo hilo la kiuchumi la Dongo Kundu kwa ajili ya kuanzisha kiwanda cha kusafisha mafuta.

Kulingana na halmashauri ya bandari nchini KPA hatua hiyo italeta faida Zaidi ikiwemo kubuni nafasi za ajira, ikuaji wa uchumi, upatikanaji wa vifaa vya baharini, na urahisi wa kufikia masoko ya kanda na ya kimataifa.

Taarifa ya Pauline Mwango

Continue Reading

Business

KETRACO kuimarisha usalama wa chakula nchini

Published

on

By

Shirika la usambazaji umeme nchini, KETRACO, limethibitisha dhamira yake ya kuimarisha usalama wa chakula, ukuaji wa kijani, na ushirikiano wa kieneo kupitia uekezaji mkubwa katika miundombinu ya umeme.

Katika maonesho ya Kimataifa ya kilimo ASK yanayoendelea kaunti ya Mombasa, KETRACO imeonyesha jinsi miundombinu yake ya umeme inavyowezesha kilimo cha kisasa na uzalishaji wa viwandani.

Kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi mkuu, mhandisi Kipkemoi Kibias, KETRACO imekamilisha miradi 43 ya njia za kusafirisha umeme, huku mingine 29 ikitarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2028.

Kibias, alisema shirika hilo tayari limejenga zaidi ya kilomita elfu sita za njia za umeme wa msongo mkubwa, likiwa pia na vituo 46 vya kusambaza umeme na upanuzi wa mitambo 33.

Katika eneo la Pwani, Kibias alisema upanuzi wa mpango wa Green Energy Backbone umewezesha usambazaji wa kawi safi kwa asilimia 93, jambo lililopunguza utegemezi wa mafuta na kuchochea maendeleo ya biashara za kilimo, utalii na uchumi wa baharini.

Kibias alisema KETRACO inaendelea kuwekeza katika teknolojia za kisasa na kuunganisha Kenya na nchi jirani kupitia njia za kimataifa kama zile za Ethiopia, Tanzania na Uganda hatua zitakazowezesha biashara ya umeme Afrika Mashariki.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Continue Reading

Trending