Connect with us

Sports

Mbeumo Akabidhiwa Jezi Namba 19 United, Baada Ya Kuzinduliwa Rasmi

Published

on

Manchester United imethibitisha kukamilisha usajili wa mshambuliaji, Bryan Mbeumo kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 71 pamoja na nyongeza akitokea Brentford na atavaa jezi namba 19 klabuni hapo.
Mbeumo (25) raia wa Cameroon amemwaga wino kwa mkataba wa miaka mitano utakaombakisha klabuni hapo mpaka Juni 2030 na chaguo la ongezeko la mwaka mmoja zaidi.
Msimu uliopita nyota huyo alikuwa mfungaji bora namba nne kwenye Ligi Kuu England nyuma ya Salah (29), Isak (23) na Haaland (22) akipachika jumla ya magoli 20 na kusaidia ‘assists’ mengine 8.
Mbeumo anakua sajili wa pili kwa kocha Ruben Amorim baada ya usajili wa mshambulizi Matheus Cunha kutoka kilabu ya Wolves.
#Kipenga
Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Sports

Gyokeres Sasa Ni Mali Ya Arsenal

Published

on

By

Klabu ya Arsenal imefikia makubaliano na Sporting Lisbon juu ya kumsajili mshambuliaji Victor Gyokeres kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 63.5 na nyongeza ya milioni 10.

Gyökeres, 27, raia wa Sweden anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano utakaombakisha kwa Washika Mitutu hao mpaka Juni 2030.
Kumekuwepo na sintofahamu kuhusiana na uhamisho huo baada ya Kilabu ya Manchester United kujaribu kupokonya Arsenal Mshambulizi huyo Ila Mshambulizi huyo alisalia kwamba anataka Arsenal pekee.
Mchezaji huyo anakua sajili wa tano kwa The Gunners baada ya usajili wa kipa Kepa Arrizabalaga,kiungo Martin Zubimendi,Christian Norgard na Mosquera.
Continue Reading

Sports

Tanzania Kupitia Wizara Ya Michezo Yaanza Hamasa Kwa Mashabiki Kuelekea Chan

Published

on

By

Hamasa za mashabiki wa Taifa Stars kuelekea michuano ya CHAN 2024 itakayoanza Agosti 2,2025 rasmi zimezinduliwa leo Julai 22,2025 viwanja vya Mbagala Zakhem.
Taifa la Tanzania kupitia kwa Wizara ya michezo hii leo imeanzisha hamasa za michuano ya Chan ambayo inangoa nanga Agosti 2 ugani Benjamin Mkapa nchini Humu.
Shughuli hiyo kulingana na Waziri msaidizi wa wizara ya Michezo Hamis Mwinjuma ni sehemu ya kurai mashabiki kujitokeza kwa wingi kutazama michuano hiyo na kushabikia vijana wa nyumbani timu ya Taifa Stars.
Taifa hilo linafungua kampeini yake dhidi ya Burkina Faso mechi za kundi B kabila ya kukwaruzana na Mauritania,kisha Madagascar kabila ya kufunga na Central Afrika Republic.
Continue Reading

Trending