Sports
Mashindano ya CHAN 2024 Yaingia Hatua Robo Fainali

Mashindano ya TotalEnergies African Nations Championship (CHAN) 2024 yameingia hatua ya robo fainali baada ya mechi za mwisho za makundi kukamilika hapo jana kwa msisimko mkubwa.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya CAF, mashindano makubwa yameandaliwa kwa pamoja na mataifa matatu β Kenya, Tanzania na Uganda β na yote yamefuzu robo fainali, jambo linaloendeleza hamasa kubwa ya mashindano haya barani.
Ufanisi wa wenyeji umeongeza uzito zaidi kwa kaulimbiu ya mashindano haya, βPamoja,β huku Afrika Mashariki ikijiandaa kushuhudia raundi nyingine ya viwanja vilivyojaa na mashabiki wenye shauku.
Kenya Yaongoza Kundi A Katika Debut;
Harambee Stars ya Kenya imekuwa moja ya simulizi kuu za mashindano, ikibatilisha matarajio kwa kufuzu robo fainali kwa mara ya kwanza katika historia yake ya CHAN na kuibuka kinara wa Kundi A.
Bao la dakika za mwisho la Ryan Ogam dhidi ya Zambia liliihakikishia Kenya ushindi wa 1-0 na kukamilisha alama 10 kileleni. Kikosi cha Benni McCarthy kimeruhusu bao moja pekee katika mechi nne, kikiashiria uimara wake wa kiulinzi.
Kenya sasa itasalia Nairobi kucheza dhidi ya Madagascar Ijumaa katika Uwanja wa Moi Kasarani. Kwa msaada wa mashabiki wa nyumbani na hali nzuri ya matokeo, Harambee Stars wamebadilika haraka kutoka wanyonge hadi kuwa tishio.
Tanzania Yatinga Robo Fainali Kwa Nguvu
Taifa Stars ya Tanzania pia iliibuka vinara wa Kundi B kwa alama 10, ikipata ushindi mara tatu na sare moja. Kikosi hiki kiliwasisimua mashabiki kwa mashambulizi makali na uthabiti, huku kiporo pekee kikiwa sare dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Tanzania sasa itakutana na Morocco Ijumaa jioni jijini Dar es Salaam. Atlas Lions, mabingwa mara mbili wa CHAN, waliibuka wa pili katika Kundi A nyuma ya Kenya.
Uganda Yavunja Nuksi ya kuondolewa mapema;
Baada ya kushindwa kufuzu hatua ya mtoano mara sita mfululizo, Uganda hatimaye imepiga hatua hadi robo fainali. Sare ya mabao 3-3 dhidi ya Afrika Kusini jijini Kampala iliwatosha Cranes kuibuka vinara wa Kundi C kwa pointi saba. Penalti ya dakika za majeruhi ya Rogers Torach ilisababisha shangwe kubwa katika Uwanja wa Taifa wa Mandela.
Uganda sasa itakutana na Senegal Jumamosi usiku, mechi inayotarajiwa kuvutia umati mkubwa zaidi katika historia ya mashindano haya.
Kundi D Laamuliwa Zanzibar
Huko Zanzibar, Sudan na Senegal zilitoka sare tasa ya 0-0 na zote zikafuzu kutoka Kundi D. Sudan, ambayo haijapoteza chini ya kocha Kwesi Appiah, iliibuka kinara kwa tofauti ya mabao, huku mabingwa watetezi Senegal wakimaliza wa pili.
Sudan itasalia Zanzibar kuvaana na Algeria Jumamosi mchana, huku Senegal wakielekea Kampala kwa mtanange wao wa robo fainali dhidi ya Uganda.
Mechi za Robo Fainali
Ijumaa, 22 Agosti 2025
-
Kenya π°πͺ vs Madagascar π²π¬ β Saa 11:00 jioni, Uwanja wa Moi Kasarani, Nairobi
-
Tanzania πΉπΏ vs Morocco π²π¦ β Saa 2:00 usiku, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam
Jumamosi, 23 Agosti 2025
-
Sudan πΈπ© vs Algeria π©πΏ β Saa 11:00 jioni, Uwanja wa Amaan, Zanzibar
-
Uganda πΊπ¬ vs Senegal πΈπ³ β Saa 2:00 usiku, Uwanja wa Taifa wa Mandela, Kampala
Sports
Shirika la Kupiga Vita Dawa za Kusisimua Misuli Duniani (WADA) Lawashtaki Kenya kwa Kukosa Kutii Kanuni

Shirika la Kupambana na Matumizi ya Dawa za Kusisimua Misuli Duniani (WADA) siku ya Alhamisi limeshtaki Kenya kwa kutotii masharti yake, hatua inayoweza kusababisha nchi hiyo ya Afrika Mashariki kuwekewa vikwazo mwezi ujao.
WADA, lenye makao yake Montreal, Canada, limesema kuwa shirika la kitaifa la kudhibiti matumizi ya dawa za kusisimua misuli nchini Kenya bado halijashughulikia mahitaji muhimu yaliyoainishwa baada ya ukaguzi uliofanywa mwezi Mei 2024.
Kwa sasa, Kenya ina siku 21 za kupinga madai hayo au kufanya marekebisho yanayohitajika na WADA, la sivyo itatangazwa rasmi kuwa imekosa kutii kanuni.
Kwa sasa, kuna wadau wanne waliotia saini kanuni za WADA walioko kwenye orodha ya kutotii masharti. Hawa ni pamoja na:
-
Urusi
-
Sri Lanka
-
Shirikisho la Kimataifa la Basque Pelota
-
Shirikisho la Kimataifa la Mazoezi ya Mwili na Ujenzi wa Misuli (IFBB)
Sports
Mkurugenzi Mkuu wa Cricket Kenya Ronald Bukusi Afafanua Hali ya Ukocha katika Timu ya Taifa

Mkurugenzi Mkuu wa Cricket Kenya, Ronald Bukusi, ameondoa uvumi kuhusu mpangilio wa uongozi ndani ya timu ya taifa ya kriketi ya wanaume, akisisitiza kuwa hakuna mkanganyiko wowote kuhusu majukumu ya makocha Joseph Angara na Lameck Onyango.
Akizungumza katika makao makuu ya shirikisho hilo Ruaraka, Nairobi, Bukusi alieleza kuwa benchi la kiufundi linafanya kazi kwa mshikamano, huku wachezaji hao wa zamani wa kimataifa wakikamilishana katika uwezo wao.
βTuna makocha wawili. Inategemea tu wanachofanya siku hiyo maalum,β alisema Bukusi.
Kwa sasa, Angara ndiye kocha mkuu, huku Onyango akiwa msaidizi wake. Wawili hao walichukua majukumu hayo kwa muda tangu Septemba 2024 baada ya bodi kufuta uteuzi wa mchezaji wa zamani wa India, Dodda Ganesh, kwa sababu za ukiukaji wa taratibu.
Kwa kuzingatia kuwa mashindano ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la ICC la 2027 yanakaribia, Bukusi alisisitiza kuwa timu ya taifa imedhamiria kazi iliyo mbele yao. Mashindano hayo makubwa duniani yataandaliwa kwa pamoja na Afrika Kusini, Zimbabwe na Namibia.
βKwa sasa, malengo yetu ni kujaribu kufika Zimbabwe na kufuzu Kombe la Dunia,β alisema Bukusi. βTuna benchi bora la kiufundi linaloongozwa na Bw. Tariq [mwanabodi], na kwa pamoja tunashughulikia changamoto zinazoikumba timu.β
Hata hivyo, alionya kuwa mafanikio yanahitaji zaidi ya kipaji cha uwanjani, akisisitiza umuhimu wa uwajibikaji na utiifu wa kanuni katika mifumo yote.
βLazima tuwe watiifu kuhusu fedha na kupiga vita matumizi ya dawa za kusisimua misuli. Sio kitu cha kufanikisha mara mojaβitakuwa mchakato,β aliongeza.
Kenya itaendeleza kampeni ya kufuzu kwa kuikabili Namibia Septemba 26 katika Harare Sports Club, kisha kucheza dhidi ya Malawi Septemba 28 katika Takashinga Cricket Club. Mechi yao ya mwisho ya makundi itakuwa dhidi ya Nigeria Septemba 30.
Kenya inatarajia kurudia historia ya mwaka 2003, walipofika nusu fainali, mafanikio makubwa zaidi kuwahi kupatikana na taifa lisilocheza mechi za Test.