News
Manchester United Ndaani Ya Fainali Europa

Miamba wa Uingereza kilabu ya Manchester United imetinga kwenye fainali ya Europa ligi msimu huu kishindo bila kupoteza hata mechi moja.
Haya yanajiri baada ya vijana wa Kocha Ruben Amorim kuinyuka kabla ya kutandika sawa sawa kilabu ya Athletico Bilbao kichapo cha magoli 4-1 na jumla ya magoli 7-1
Wageni walichukua uongozi wa mapema kupitia kiungo Mikel Juregizer dakika ya 31 kipindi cha kwanza ,hata hivyo mashetani wekundu hao walirejea kwa moto wa radi kipindi cha pili wakijipatia magoli yao kupitia kiungo muingereza Mason Mount dakika ya 71 kabila ya Kiungo Casemiro kuongeza la pili dakika ya 80 huku mshmabulizi Rasmus Hojlund akicheka na nyavu dakika ya 85 na Mount Kuongeza lake la Pili na la nne kwa United dakika ya 93.
Katika matokeo mengine Tottenham Hotspurs walinyuka Bodo/Glimt 2-0 na jumla ya magoli 5-1 na sasa fainali ni kati ya timu za Manchester United na Spurs Ugani San Mames Uhispania Mei 21.
News
Mzozo kati ya Kenye na Tanzania waendelea kutokota

Serikali ya Kenya imeiandikia barua jumuiya ya afrika mashariki kupinga vikwazo vilivyowekwa na Tanzania kuhusu kufanya biashara katika taifa hilo.
Katibu mkuu katika idara ya EAC Daktari Caroline Karugu, alisema kenya imebaini kuwa agizo hilo haliambatani kamwe na masharti muhimu ya itifaki ya soko la pamoja la EAC, ambayo inahakikisha uruhu wa watu kusafiri, kuhudumu na haki ya kuanzishwa kwa biashara na raia wa mataifa ya afrika mashariki.
Aidha Kenya iliasema imeandika rasmi barua kwa EAC kuiarifu rasmi jamhuri ya muungano wa Tanzania kuangazia upya agizo hilo ili kuhakikisha inafuata kikamilifu mkataba wa EAC na sheria za Jumuia.
Maafisa wa EAC kwa sasa wanafanya uchambuzi wa hatua hiyo na itawasilisha hatua zozote zilizokiukwa pamoja na kaununi zilizopo katika mkutano ujao wa baraza la kisekta la biashara, viwanda na uekezaji.
Taarifa ya Joseph Jira
News
Mradi wa Galana Kulalu kukabili uhaba wa chakula nchini

Serikali imesema inalenga kufikia ekari 3,200 za kilimo katika mradi wa uzalishaji chakula wa Galana Kulalu ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2025.
Waziri wa maji, usafi na kilimo nyunyizi Eric Mugaa alisema tayari ekari 1,060 zimepandwa mahindi kwa kutumia mifumo ya umwagiliaji ya kisasa, mazao ya kwanza yakitarajiwa kuvunwa mwezi Oktoba, huku maandalizi yakuongeza mashamba zaidi yakiendelea.
Akizungumza alipozuru mradi wa Galana Kulalu kutathmini maendeleo ya shughuli za mradi huo, waziri Mugaa pia alisema miundombinu mipya ikiwemo mabwawa ya kuhifadhi maji, mifareji ya kunyunyiza maji, na mitambo ya kusukuma maji imejengwa ilikuwezesha shughuli za unyunyizaji.
Wakati huo huo, waziri huyo alidokeza kuwa ujenzi wa Daraja la Sabaki umefikia hatua ya asilimia 50, akidokezakwamba daraja hilo linatarajiwakukamilika hivi karibuni ili kurahisisha usafirishaji wa vifaa vya kilimo na vile vilekusafirisha mazao kutoka Galana Kulalu.
Serikali kupitia Mamlaka ya unyunyizi iliahidi kuendelea kushirikiana na sekta za kibinafsi kuhakikisha mradi huo wa Galana Kulalu unakuwa suluhu ya uhaba wa chakula hapa nchini.
Taarifa ya Mwanahabari wetu