Connect with us

News

Mahakama yasitisha ujenzi wa kanisa katika Ikulu ya Rais

Published

on

Mahakama imesitisha ujenzi wowote wa kanisa la kudumu au hata maeneo ya ibada unaoweza kuendeshwa katika ikulu ya rais kwa sasa.

Mahakama pia ilisitisha ujenzi wa maeneo haya ya ibada kwenye ikulu ndogo zote nchini.

Jaji Chacha Mwita alitoa uamuzi huo kufuatia kesi iliyowasilishwa na mashirika ya kutetea haki za binaadam, ikiibua maswali kuhusu sheria, dini na majukumu ya serikali.

Walalamishi kwenye kesi hiyo walisema kuanzishwa kwa miundo mbinu ya kidini kwenye maeneo ya umma kama ikulu, kunaashiria ukiukaji mkubwa wa katiba.

Hatua ya kujengwa kwa kanisa katika ikulu ya rais iliibua hisia mseto nchini huku baadhi ya wananchi na viongizo wa dini wakipinga hatua hiyo.

Walidai hatua hiyo inaenda kinyume na sheria za taifa.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 18 Novemba mwaka wa 2025.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Mawakili Kilifi waungana kushtumu mauaji ya Wakili Mbobu

Published

on

By

Siku chache baada ya Wakili Kyalo Mbobu kuuawa kinyama kwa kupigwa risasi mara kadhaa akiwa kwenye gari lake barabara ya Lang’ata jijini Nairobi, mawakili mjini Kilifi kaunti ya Kilifi wameungana na mawakili wengine nchini siku ya Ijumaa Semtemba 12 mwaka huu kufanya matembezi ya amani, wakishutumu vikali mauaji hayo.

Wakiongozwa na Mwakilishi wao Sesil Mila, mawakili hao walilaani vikali mauaji ya wakili Mbobu wakiishutumu serikali kwa kutowajibikia swala la usalama wa wananchi wake.

Aidha waliitaka idara ya usalama kuhakikisha kuwa inafanikisha wajibu wake wa kuwalinda mawakili wakisisitiza haja ya haki kupatikana kwa familia ya mwendazake wakili Kyalo.

Mawakili wa Kilifi wakiongozwa na Sesil Mila, washtumu mauaji ya Wakili Kyalo Mbobu

Mawakili hao sasa waliitaka idara ya upelezi na asasi zote husika kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina unafanywa kubaini watuhumiwa wa mauaji hayo ili wachukuliwe hatua kali za kisheria haraka iwezekanavyo.

Taarifa ya Hamis Kombe

Continue Reading

News

IEBC inaendelea kutambua vituo vya kusajili wapiga kura

Published

on

By

Maafisa wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC wamesema wanaendelea na zoezi la kutambua sehemu za kuweka vituo vya kusajili wapiga kura hasa maeneo ya mashinani.

Afisa msimamizi wa tume ya IEBC eneo bunge la Ganze kaunti ya Kilifi, Mohammed Bahero Aboud alisema juhudi hizo ni kuhakikisha zoezi la usajili wapiga kura litakaloanza rasmi Septemba 29, mwaka huu linafaulu.

Akizungumza mjini Kilifi, Bahero alisema tume hiyo inatumia mbinu mpya ya kutambua vituo vya jadi vya usajili wapiga kura na kuweka vituo vipya kulingana na mapendekezo ya sheria.

Wakati huo huo alidokeza kwamba tume ya IEBC imekuwa ikihamashisha wakenya kutokubali kushawishiwa na wanasiasa na kujisajili katika maeneo yasiokuwa yao hasa msimu huu ambao zoezi hilo linakaribia kuanza.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading

Trending