News
Maafisa wa Polisi Wamewakamata Wahalifu 9, Mtwapa.

Maafisa wa usalama eneo la pwani wanasema wamewakamata wanaume 9 wa umri kati ya miaka 26 hadi 30 kwa tuhuma za wizi eneo la Mtwapa kaunti ya Kilifi.
Kulingana na polisi washukiwa walikamatwa na mali ya uizi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 7 katika nyumba wanamoishi.
Kamanda wa polisi hapa pwani Ali Nuno alisema maafisa wa polisi wamefanikiwa kupata magari nane yanayodaiwa kuwa ya wizi, baadhi yakiaminika kutumika na washukiwa kutekeleza shughuli hizo.
Nuno alidokeza washukiwa wamekuwa wakiwawinda watu wanaotoka kutoa pesa kwenye benki na kuwaibia kwa kutumia vifaa maalumu vya kufungua magari wakati wanapoziwacha pesa hizo ndani ya gari.
Nono vile vile alidokeza kuwa baadhi ya washukiwa waliokamatwa ni wezi sugu na ambao wanaripoti za kihalifu zilizoripotiwa tangu mwaka 2017 katika mahakama ya Mombasa.
Taarifa ya Joseph Jira
News
Godhana, awataka wakaazi kutoingiza siasa miradi ya maendeleo

Gavana wa kaunti ya Tana River Dhadho Godhana amewataka wenyeji wa kaunti hiyo kujiepusha na wanasiasa ambao wanaingiza siasa kwenye masuala ya maendeleo.
Godhana alisema hilo limechangia kaunti ya Tana River kusalia nyuma kimaendeleo hali ambayo itasababisha miradi mingi kuzidi kukwama.
Godhana alisema ni lazima viongozi na wenyeji wa kaunti ya Tana River washirikiane na uongozi wa kaunti ili kuafikia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Wakati huo huo Godhana aliesema mradi wa Village Cluster ambao umekuwa ukipingwa ndio utakaosaidia kudhibiti changamoto ambazo zinaikumba kaunti ya Tana River.
Naye Mahat Ali Loka ambaye ni Naibu Gavana wa kaunti ya Tana River, aliwaonya wanasiasa kutoka kaunti zingine dhidi ya kuingilia siasa za kaunti hiyo huku Spika wa bunge la kaunti hiyo Osman Noor Galole, akitoa onyo kwa wafanyikazi wa umma dhidi ya kujumu la serikali ya kaunti ya Tana River.
Taarifa ya Janet Mumbi
News
Mwili wapatikana baharini Shelly Beach Likoni

Polisi kaunti ya Mombasa wanachunguza kisa ambapo mwili wa mwanamme ambaye hajafahamika umepatikana ukielea katika maji ya bahari hindi kwenye ufuo wa Shelly Beach eneo bunge la Likoni.
Ripoti ya polisi ilibaini kuwa mwili huo uligunduliwa na wavuvi eneo hilo, ambao walipiga ripoti katika kituo cha polisi cha Shelly Beach kuhusiana na tukio hilo.
Polisi walisema hawakubaini mara moja anakotoka mtu huyo.
Vile vile haikubainika iwapo marehemu alizama au aliuawa kabla ya mwili wake kutupwa baharini.
Polisi walisema hawajakutana na stakabadhi zozote za kumtambulisha mtu huyo huku wakiwasihi wananchi kutoa taarifa iwapo wanafahamu familia ya marehemu.
Mwili unahifadhiwa katika hifadhi ya maiti katika hospitali ya Rufaa ya Coast General Mombasa wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.
Taarifa ya Joseph Jira