Connect with us

Sports

Liverpool Yakubaliana Dili Ya Kerkez

Published

on

Kilabu ya Liverpool imekubaliana na AFC Bournemouth kuhusiana na uhamisho wa pauni milioni 4o kwa beki Milos Kerkez raia wa Serbia.

Tineja huyo anatarajiwa kuwasili Liverpool muda wowote kufanyiwa vipimo vya kimatibabu na kumwaga wino mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa ligi kuu Uingereza.

Mchezaji huyo alikua nguzo muhimu kwa kilabu ya Bournemouth wakimaliza kumi bora akichangia magoli matano na kufunga mawili,anakua sajili wa tatu kwa kocha Arne Slot kwenye kilabu hio.

The Reds wakiwa wametumia pauni milioni 116 kumpata kiungo Florian Wirtz,pauni milioni 31 kupata Jeremie Frimpong.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Sports

Starlets Kucheza Fainali Ya CECAFA Dhidi Tanzania

Published

on

By

Kikosi cha soka akina dada kushuka dimbani kucheza dhidi ya Twiga Stars Ya Tanzania kwenye fainali ya kipute cha CECAFA Afrika Mashariki ugani Azam Sports Complex.

Vipusa wa kocha Beldine Odemba wameshinda mechi zote tatu ikiwemo kuwalaza Sudan Kusini magoli 4-0 mechi ya siku ya Alhamisi huku wakiwa wamekusanya alama 9 sawa na wenyeji Tanzania kwenye mashindano ya mwaka huu.

kwa mujibu wa mwalimu huyo wanatarajia mechi ngumu dhidi ya wapinzani wao kwani wako nyumbani na timu bora pia.

“Tuko tayari kwa mechi ya mwisho ambayo pia ni fainali kila mmoja anajua tumekua vizuri katika mashindano haya ila Tanzania ni mpinzani mkubwa katika fainali ya leo kwa sababu pia hawajapoteza mechi kama sisi.”

Mechi hiyo inangoa nanga saa 12.00 jioni.

Continue Reading

Sports

Fainali Ya Chan 2025 Kupigwa kenya

Published

on

By

Shirikisho la kandanda Barani Afrika CAF imethibitisha kwamba mji wa Nairobi atakua mwenyeji wa fainali ya  kombe hilo ambalo linaandaliwa na nchi tatu za Afrika Mashariki Kenya,Uganda na Tanzania.
Miji ambayo itaanda fainali ya Chan mwaka 2024 ni kama ifuatavyo;
Dar es Salaam  – Mechi Ya Ufaunguzi
Kampala  – Mechi Ya Mshindi wa Tatu
Nairobi  – Mechi Ya Fainali
Miji ambayo itaanda mechi za makundi:
Kundi  A | NAIROBI: Kenya, Morocco, Angola, DR Congo, Zambia
Kundi  B | DAR ES SALAAM: Tanzania, Madagascar, Mauritania, Burkina Faso, Central African Republic
Kundi C | KAMPALA: Uganda, Niger, Guinea, South Africa, Algeria
Kundi D | ZANZIBAR: Senegal, *Congo, Sudan, Nigeria
#CHAN2025
Continue Reading

Trending