Connect with us

News

Kina mama wajawazito na waliojifungua kwenye hospitali ya rufaa mjini Kilifi, wapokea zawadi kutoka Coco Fm

Published

on

Uhaba wa wauguzi ni miongoni mwa changamoto ambazo zinatatiza shughuli za utoaji wa huduma za matibabu katika hospitali ya rufaa mjini Kilifi kaunti ya Kilifi.

Wakizungumza na Coco Fm, baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa Mjini Kilifi wakiongozwa na Nyadzua Pandau wamesema hali hiyo inawafanya kulazimika kufanya kazi  kupita muda unaohitajika kwani idadi ya wagonjwa wanaohitaji matibabu ni kubwa kuliko ile ya wauguzi waliopo kwenye hospitali hiyo.

Vilevile, wametaja ukosefu wa dawa kwenye hospitali hiyo na kutoa wito kwa serikali ya Kaunti ya Kilifi kuhakikisha zinapatikana ili wagonjwa watibiwe bila changamoto zozote.

Aidha, wauguzi hao wameitaka serikali ya kitaifa pamoja na ya kaunti ya Kilifi kuwekeza zaidi katika kuimarisha huduma za matibabu na kukishukuru kituo cha COCO FM kwa kutoa zawadi kwa kina mama hospitalini humo jana wakati wa siku ya Kina duniani.

 

Continue Reading
Click to comment

0 Comments

  1. Thomaskombe

    May 13, 2025 at 1:28 pm

    Coco fm radio ina matangazo bora
    Twaomba itufikie huku mitaani kweku
    Magarini naviungani maana tuna hitaji matangazo na burudani
    Na vipindi vya salamu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Mwanaharakati Mwabili Mwagodi apatikana

Published

on

By

Mwanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu Mwabili Mwagodi ambaye alidaiwa kutekwa nyara akiwa nchini Tanzania sasa amepatikana.

Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za kibinamu nchini la VOCAL Africa Hussein Khalid, alisema Mwabili alipatikana katika msitu wa Kinondo eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale mwendo wa saa tisa usiku akitembea kuelekea Diani.

Khalid alisema Mwabili, anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Pandya mjini Mombasa kisha baadaye atasafirishwa kwa ndege hadi jijini Nairobi kuungana na familia yake.

“Tunashukuru Mwabili amepatikana akiwa hai japo amedhohofika na anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Pandya na kisha atarudi Nairobi kukutana na familia yake lakini tunaiambia serikali ya Kenya na Tanzania ni lazima wahusika kukomesha tabia hii ya kuwateka watu nyara kuna sheria kama mtu amekosea apelekwe Mahakamani”, alisema Khalid.

Hata hivyo Wanaharakati hao wa kutetea haki za kibinadamu waliishtumu serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuwanyanyasa wanaharakati wa kijamii wa taifa la Tanzania na wale wanaoingia Tanzania kutoka mataifa mengine ili kuendeleza hamasa za haki za kijamii.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Continue Reading

News

Kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Herman yahairishwa

Published

on

By

Kesi ya mauaji ya mfanyabiashara ambaye ni raia wa Uholanzi, Rowenhorst Herman na mlinzi wake Evans Bokoro imeahirishwa hadi mwezi Oktoba mwaka huu kufuatia Mahakama kuingia kwenye mapumziko rasmi ya majaji.

Mke wa Marehemu, Riziki Cherono pamoja na mshukiwa mwenza Timothy Omondi wanakabiliwa na mashtaka ya kupanga na kutekeleza mauaji hayo yaliyotokea Juni 4 mwaka 2021 katika eneo la Shanzu kaunti ya Mombasa.

Katika kikao cha awali cha Mahakama, Afisa wa Polisi Koplo Richard Cheruiyot alieleza mbele ya Jaji Wendy Micheni kwamba Cherono alijaribu kuonekana kama mwathirika kwa madai ya kutekwa nyara na majambazi waliodaiwa kuvamia nyumba yao.

Afisa huyo alieleza kwamba walimkuta Cherono akiwa amefungwa kwenye usukani wa gari lake, huku akidai kwamba alivamiwa na kulazimishwa kuondoka nyumbani kwao akiwa chini ya tishio la bunduki.

Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa ulibaini kwamba Marehemu Herman alipatikana amefariki nyumbani kwake akiwa amefungwa mikono na miguu huku mlinzi wao, Evans Bokoro, alikutwa akiwa hai kwa taabu karibu na bwawa la kuogelea lakini baadaye alifariki akipelekwa hospitalini.

Mashahidi wa upande wa mashtaka pamoja na polisi, wanaamini kwamba Cherono ndiye mshukiwa mkuu wakidai kwamba alipanga na kufanikisha mauaji hayo kwa kushirikiana na watu wengine, wakiwemo waliotajwa kuwa sehemu ya genge lililovamia nyumba hiyo.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Continue Reading

Trending