Sports
Kocha Wa Starlets Odemba ajiuzulu

Mkufunzi wa timu ya taifa soka akina dada Harambee Starlets Beldine Odemba ametangaza kujizulu wadhifa wake kama kocha mkuu wa kikosi hicho baada ya kichapo cha magoli 5-1 na Morocco mechi ya kirafiki.
Kwa mujibu wa mwalimu huyo kilichomfanya kuondoka katika kambi ya timu hiyo ni kukosa ungwaji mkono katika kazi yake ya kunoa starlets akiondoka siku chache tuu kabla ya kungoa nanga kwa taji Cecafa nchini Tanzania Juni 12.
Mkufunzi huyo ambaye ameshinda ligi ya akina dada na kilabu ya Kenya Bullets amedokeza kwamba ni swala ambalo ameliwazia kwa muda na kwa sasa anaelekeza nguvu zote kwa kikosi hicho taji la Cecafa baina ya vilabu.
Ripoti zinaarifu kwamba kocha wa Kibera Soccer Women David Vijago atatangazwa kocha mpya wa Starlets akisaidiana na Alex Alumira ambaye amewahi kuwa kocha wa timu hiyo.
Sports
Liverpool Kuwasilisha Ofa Mpya Kusajili Wirtz

Mabingwa wapya wa ligi ya Epl liverpool inatarajiwa kuwasilisha ofa nyingine kusaka hudumza kiungo matata wa Ujerumani Florian Wirtz.
Hii ni Baada ya kilabu ya Bayer Leverkusen kukataa ofa ya pauni milioni 113 kutoka kwa usajli wa mchezaji huyo ambaye ameweka wazi yuko tayari kujiunga na The Reds msimu ujao.
Leverkusen imeshikilia kuwa inahitaji kitita cha pauni milioni 126 kumwachilia nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye pia anamezewa mate na Real Madrid ya Uhispania na Manchester City wa Uingereza.
Inaaminika mchezaji huyo ndiye atakua sajili wa kwanza kwa kocha mkuu Arne Slot msimu huu wakiwa tayari kuwachiliwa nyota wake akiwemo mshmabulizi Darwin Nunez,Federico Chiesa,Harvey Elliot na Kostas Tsimiskas ambao wote wataondoka ugani Anfield.
Sports
Kenya Pipeline Ndiyo Mabingwa Voliboli Akina Dada

Kilabu ya Kenya Pipeline ndiyo mabingwa wa taji la akina dada ligi ya Voliboli baada ya kushinda kilabu ya DCI seti 3-2 (21-25, 25-21, 18-25, 25-21, 15-11) fainali kali iliopigwa ugani Kasarani Indoor Arena wikendi.
Kulingana na Kocha mkuu George Omondi amefurahishwa na matokeo hayo licha ya upinzani kuwa mkali zaidi,
“Tulihitaji Kucheza vizuri mpaka mwisho,Tulijua ni lazima tucheze kwa ukakamavu mkubwa kwani si mechi rahisi katika fainali ila wasichana wangu wamekakamua kufanya kweli na kuvuna ushindi huu ambao ni wa kipekee.”
Kocha wa DCI Patrick Sang aliweza kushukuru wapinzani wake kwa kushinda hata hivyo akishikilia kufika katika fainali si jambo jepesi tangu wajaribu kwanzia mwaka 2018.
“Nimeridhika na Matokeo wasichana hao wamecheza kwa ushujaa mkubwa tulitaka taji ila nimeridhika na nafasi ya pili kuwa nafasi ya pili si mabya kwetu ni matokeo bora zaidi.”
Upande wa wanaume kinyanganyiro ni kati ya GSU na KPA.