Sports
Kilabu Ya Kenya Police Mabingwa Ligi Kuu FKF PL

Timu ya Kenya Police FC imetawazwa mabingwa wa Ligi Kuu ya FKF kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake, katika mechi ya mwisho dhidi ya Gor Mahia iliyopigwa kwenye Uwanja wa Ulinzi Sports Complex, .
AFC Leopards 0-0 KCB,BANDARI 1-1 POSTA,KAKAMEGA HOMEBOYZ 0-0 TUSKER,KSHARKS 4-1 MARA SUGAR,SHABANA 1-1 ULINZI STARS,MURNGA 1-0TALANTA,Shabana 1-1 Ulinzi Stars,Nairobi City Stars 0-0 Mathare United ,Sofapaka 1-2 Bidco United.
Vilabu vya Niarobi City Stars na Talanta vimeteremshwa ngazi huku Posta Rangers ikimaliza nafasi ya 16 na sasa italazimika kucheza mechi ya mchujo dhidi ya timu ya tatu ya ligi ya daraja ya pili NSL.
Sports
Kikosi Cha Taifa Mchezo Wa Netiboli Yashinda Shaba-UAE

Kikosi cha Taifa kwa akina dada mchezo wa Pete marufu kama Divas waliweza kumaliza ya tatu na kushinda tuzo la Shaba katika mashindano ya UAE Netball Championship katika milki za kiarabu.
Vipusa hao walishinda mechi ya mwisho alama 46-37 dhidi ya Ireland na kupata nishani hiyo ya shaba.
Taifa La Namibia liliweza kuwangusha mibabe na kushinda kombe hilo na tuzo la Dhahabu mechi ya mwisho kwa alama 62-53 dhidi ya taifa la Singapore.
Sports
Liverpool Yakubaliana Dili Ya Kerkez

Kilabu ya Liverpool imekubaliana na AFC Bournemouth kuhusiana na uhamisho wa pauni milioni 4o kwa beki Milos Kerkez raia wa Serbia.
Tineja huyo anatarajiwa kuwasili Liverpool muda wowote kufanyiwa vipimo vya kimatibabu na kumwaga wino mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa ligi kuu Uingereza.
Mchezaji huyo alikua nguzo muhimu kwa kilabu ya Bournemouth wakimaliza kumi bora akichangia magoli matano na kufunga mawili,anakua sajili wa tatu kwa kocha Arne Slot kwenye kilabu hio.
The Reds wakiwa wametumia pauni milioni 116 kumpata kiungo Florian Wirtz,pauni milioni 31 kupata Jeremie Frimpong.