News
Kilabu Ya Arsenal Yaboronga Uefa

Uefa
Kilabu ya PSG ya Ufaransa kucheza dhidi ya Inter ya Italia kwenye fainali ya uefa baada ya kunyamazisha kabla ya kuzimisha kilabu ya Arsenal kipigo cha magoli 2-1 ugani Parc de prince siku ya jumatano.
Kiungo wa Uhispania Fabain Ruiz aliwaweka uongozini Psg kunako dakika ya 27 kabla ya Akraf Hakimi kuweka la pili kunako dakika 72 kipindi cha pili ikawa ni jumla ya magoli 3-1
Goli la kufutia machozi la Arsenal lilitiwa kimyani ni winga wa Uingereza Bukayo Saka kunako dakika ya 76 kipindi cha pili na kuzamisha kabisa matumaini ya timu kupata taji msimu huu.
Hata hivyo baada ya kubanduliwa nje kocha wa The Gunners Mikel Arteta angali na asisitiza walikua timu bora kwenye kombe hilo huku akidai Psg walisadiwa pakubwa na kipa wao Gianluigi Donnaruma raia wa Italia aliyefanya kazi kubwa ya makombozi na kuwanyima nafasi vijana wake.
News
Wazee wa Kaya wanataka bunge kupitisha sheria kudhibiti mauaji ya wazee

Muungano wa Wazee wa Kaya kaunti ya Kilifi umeitaka serikali kuu kupitia bunge la kitaifa kubadilisha sheria ya mwaka wa 1926 kuhusu uchawi ili kuwezesha utamaduni kudhibiti mauaji ya wazee yanayoendelea kushuhudiwa kaunti ya Kilifi.
Wakiongozwa na Stanley Kahindi Kiraga wamesema kuwa sheria hiyo imechangia pakubwa mauaji ya wakongwe Kilifi kutokana na swala kuwa haitambui uwepo wa uchawi na jinsi ya kuudhibiti.
Kiraga sasa anasema ni sharti sheria hiyo iondolewe au ifanyiwe ukarabati bungeni hali itayopelekea uchawi kudhibitiwa kupitia mila na utamaduni.
“Vijana wanaowaua wazee wakiwasingizia kuwa wachawi wanazidi kuongezeka na kwa sababu hakuna sheria ya moja kwa moja ya kuwashtaki na kuwafunga” amesema Kiraga akieleza kusikitishwa kwake na ongezeko la magenge ya vijana wanaolipwa kutekelezwa mauaji ya wazee kwa shutuma za uchawi.
Taarifa ya Hamis Kombe
News
Mahakama ya Kilifi yaanzisha upya kesi ya ulaghai wa pesa

Mahakama ya Kilifi imeanzisha upya kesi ya mwanaume mmoja anayekabiliwa na shtaka la ulaghai wa pesa.
Hii ni baada ya Mwanaume huyo kwa jina Samuel Ngonyo, kuachiliwa kwa dhamana hapo awali lakini alikosa kudhuhuria vikao Mahakamani hali iliyopelekea kesi hiyo kuanzishwa upya.
Hakimu mkuu wa Mahakama hiyo Charles Obulutsa aliagiza jamaa huyo kuzuliwa rumande baada ya agizo la kukamatwa kwake kuidhinishwa na Mahakama baada ya jamaa huyo kupuuza vikao vya Mahakama vya awali.
Kabla ya agizo hilo, Mahakama ilielezwa kwamba mnamo tarehe tofauti kati ya mwezi Septemba hadi Oktoba mwaka 2021 katika maeneo la Ganze kaunti ya Kilifi kwa kutumia njia ya ulaghai, mshukiwa alichukua pesa taslimu shilingi elfu 50 ya mlalamishi Grace Sidi Katana.
Mahakama ilielezwa zaidi kwamba mshukiwa alitekeleza kitendo hicho baada kumdanganya Mlalamishi kwamba yeye ni Mwandishi na afisa wa kazi za umma hivyo angemsaidia Moses Katana mtoto wa mlalamishi kupata kazi ya serikali.
Kesi hiyo itaendelea mnamo tarehe 13 mwezi Agosti mwaka huu.
Taarifa ya Mwanahabari wetu