News
KEBS, Yawaonya Wananchi Kuhusu Bidhaa Ghushi

Shirika la kutathmini ubora wa bidhaa nchini KEBS limesema wakenya wengi wamekuwa wakinunua bidhaa ghushi ambazo hazijathibitishwa na Shirika hilo kutokana na ukosefu wa ufahamu kuhusu ubora wa bidhaa.
Shirika hilo ambalo limeandaa warsha ya siku moja na Wanahabari mjini Kilifi, kuelezea hatua zilizopigwa na Shirika hilo katika kukabiliana na bidhaa ghushi nchini, limesema juhudi hizo zitaendelezwa ili kuhakikisha bidhaa zimeafikia viwango hitajika.
Shirika hilo pia limetoa wito kwa wakenya kuwa waangalifu wanaponunua bidhaa mbalimbali kutoka kwa maduka au sokoni ili kuepuka kuuziwa bidhaa ghushi.
News
Kanisa Katoliki nchini lashinikiza maridhiano.

Kanisa Katoliki nchini limeshinikiza serikali na vijana kuridhiana ili kuepuka vurugu zaidi zinazoshuhudiwa nchini.
Askofu mkuu wa kanisa katoliki Athony Muheria wa Nyeri na Phillip Anyolo wa Dayosisi ya Nairobi, waliitaka serikali kuhakikisha wanaoathirika kwenye Dhulma za maandamano wanafidiwa.
Viongozi hao wa dini walisema kunaumuhimu wa kuthamini maisha ya binadamu na kushinikiza viongozi wa siasa kuepuka kutoa semi za kuchukiza upande wowote Ule.
Matamshi ya viongozi hao yalijiri wakati vijana wa kizazi cha Gen Z, pamoja na mashirika ya kijamii wakiendelea na maandalizi ya maandamano ya kumbukumbu ya yaliyojiri juni tarehe 25 mwaka 2025, wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha.
Wakati wa maandamano hayo baadhi ya vijana waandamamanaji walipoteza maisha, wengine kuacha na majeraha na wengine kutekwa nyara na kupotezwa katika njia tatanishi
Taarifa ya Joseph Jira
News
Seneta Madzayo amuonya Inspekta jenerali wa Polisi.

Seneta wa kaunti ya Kilifi Stewart Madzayo amemtaka inspekta jenerali wa polisi nchini Douglas Kanja kuhakikisha maandamano ya vijana wa rika la Gen z tarehe 25 mwezi juni 2025 hayashuhudii umwagikaji damu.
Madzayo ambaye pia ni kiongozi wa wachache katika bunge la seneti alimtaka Inspekta Kanja kuhakikisha maafisa wa polisi wanawalinda waandamanaji badala ya kuwadhuru.
Akizungumza eneo la Mzambarauni-Mtwapa eneo bunge la Kilifi Kusini, Madzayo alidokeza kuwa maandamano hayo yatakuwa ya amani akikumbusha vijana hao wa Gen Z kuhakikisha wanadumisha amani wakati wa maandamano hayo.
“Tumeskia tarehe 25 kutakuwa na maandamano ya amani, nataka kumwambia inspekta jenerali Kanja, tafadhali watoto wetu watakuwa katika maandamano ya amani kwa hivyo usijaribu hata kidogo kutumia polisi vibaya kuweza kuumiza watoto wetu”, alisema Madzayo.
Kwa upande wake mbunge wa eneo hilo Ken Chonga aliwaomba viongozi wa kanisa nchini kuombea taifa kutokana na visa vya mauaji na utekeji nyara vinavyoshuhudiwa nchini.
“Tumekuwa na changamoto kubwa sana kati ya upinzani na serikali hali ya maafa ikiingia, haya yote ambayo yanaendelea sa hii yote sababu ni siasa, langu ni kusihi kwanza kanisa tunahitaji maombi yenu”, alisistiza Chonga.
Maandamano hayo ya GEN Z yanatarajiwa kufanyika tarehe 25 mwezi juni 2025 kukumbuka vijana waliopoteza maisha wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha mwezi juni mwaka 2024.
Taarifa ya Joseph Jira