Sports
Kasarani Na Nyayo:Uwezo Wa Kubeba Mashabiki Yapungua

CHAN Siku 17 zimesalia kipute hicho kungoa nanga nchi za Kenya,Uganda na Tanzania.
Serikali ya Kenya kupitia Wizara ya Michezo imetumia Kima Cha zaidi ya Shilingi Bilioni 6.7 kufanyia Ukarabati uwanja wa Kasarani na Shilingi nyingine Bilioni 1.1 Uga wa Nyayo.
Sports
Rais Ruto Awapa Morale Kikosi Cha Stars Kambini

Rais William Samoei Ruto mapema Leo ametembelea kikosi Cha timu ya Taifa Mpira wa Soka Harambee Stars Ugani Kasarani wanapofanyia mazoezi kwa Kombe la Chan 2025 mwezi ujao.
Hii ikiwa ni njia moja wapo ya kuwapa mortisha vijana wa nyumbani akiahidi Stars nchi nzima iko nyuma Yao.
Ruto amewatakia heri Stars na kuambia vijana wa nyumbani watapata sapoti yoyote wanayohitaji kutoka kwake wanapo peperusha bendera ya taifa hili kwenye kipute cha CHAN mwezi ujao.
“Nataka tushinde kombe hili katika nchi yetu,kila Mkenya yuko nyuma yenu kuwapiga jeki ili mpate matokeo chanya mimi na serikali yangu tunahidi kuwapa sapoti yote kwa kombe hili.”
Rais aliandamana na Waziri wa Michezo Salim Mvurya pamoja na waziri wa Ulinzi Soipan Tuya.
Vijana wa nyumbani wanafungua kampeini Agosti 3 dhidi ya DR. Congo ugani Kasarani ambapo watapiga mechi zao zote.
Sports
Kenya Yafinya Mashabiki Wake Kwenye Tiketi Za Chan Agosti.
