Sports
Harambee Stars Kundi La Kifo Kundi B.

Huku zikiwa zimesalia siku 15 pekee kung’oa nanga kwa kipute cha CHAN mwezi ujao,
Kenya imeratibiwa kupambana na DRC, Morocco, na Angola katika Kundi A linalotajwa kuwa ndio kundi gumu zaidi yaani Kundi la Kifo.
KUNDI B
Ni Taifa jirani la Tanzania, Burkina Faso, Madagascar na Jamhuri ya Africa ya Kati.
KUNDI C
Uganda itachuana na Algeria,Africa Kusini,Guinea na Nigeria.
KUNDI D:
Congo itakabana koo na Nigeria,Senegal na Sudan Kusini.
Mechi hizi zitasakatwa katika nyuga za katika Kenya, Uganda na Tanzania,
Continue Reading
Sports
Kiungo Wa Brenford Bryan Mbeumo Sasa Ni Mali Ya United

Baada ya vute ni kuvute ambayo imedumu kwa kipindi cha mwezi mmoja ni rasmi kwamba kilabu ya manchester United na Brenford wameafikia makubaliano ya pauni milioni 70 ya kiungo mshambulizi Bryan Mbeumo raia wa Cameroon.
Haya yanajiri baada ya ofa mara mbili ya united kukataliwa na kilabu hio kabila ya kutuma ofa ya mwisho ya pauni milioni 65 na nyongesa ya pauni milioni 5.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 yuko tayari kumwaga wino mkataba wa miaka mitano baada kukubali matakwa yake binafsi.
Mbeumo anakua sajili wa pili kwa kocha mkuu Ruben Amorim baada ya ujio wa mshmabulizi Matheus Cunha.
Sports
Twende Kasarani Tushabikie Stars- Asema Waziri Mvurya

Waziri wa michezo Salim Mvurya ametangaza kwamba matayarisho ya michuano ya CHAN yamekamilika na vijana wa nyumbani wako tayari kuakilisha Taifa.
Kenya itatumia viwanja vya Kasarani, na Nyayo, huku viwanja vya Polisi SACCO, Kasarani Annex na Ulinzi sports Complex, vikitumika Kwa mazoezi ya timu zote zinazoshiriki michuanobuii.
Akizungumza mjini Kilifi, Waziri Mvurya aliwahakikishia Wakenya burudani huku akiwaalika kujitokeza Kwa wingi kushabikia timu ya Taifa Harambee Stats.
Ukarabati wa Viwanja hivi viwili umekamilika hivi majuzi na kukabidhiwa rasmi Kwa Kamati andalizi ya michuano hiyo kwenye hafla iliyohudhuriwa na Waziri wa Usalama Kipichunba Murkomen na Waziri Mvurya.
Timu ya Taifa Harambee stars itafungua dimba hilo ikiwa katika Kundi A pamoja na DR Congo, Morocco, Zambia na Angola. Kundi hili kimetajwa kuwa gumu zaidi.