Staa wa Bongo Fleva Alikiba ameibua mjadala mzito kufuatia kauli yake aliyoitoa baada ya kufanya show kubwa na yenye mafanikio jijini Mwanza, nchini Tanzania.
Baada ya kupanda jukwaani na kuonesha kiwango chake cha juu cha uimbaji na burudani, King Kiba aliacha mashabiki wakizungumza zaidi si tu kuhusu show yake, bali pia kauli yake iliyokuja mwishoni mwa performance yake. Akiwa mbele ya umati mkubwa wa mashabiki, alisema kwa kujiamini:
āWatatoa ngoma nyingine na nyingine, na nyingine, na nyingine, na nyingine⦠halafu mimi natoa nyingine, moja tu.ā
Kauli hiyo imezua tafsiri mbalimbali miongoni mwa mashabiki na wadau wa muziki, wengi wakiona kuwa ni ujumbe unaolenga tofauti iliyopo kati ya wasanii wanaotoa kazi nyingi kwa wakati mfupi na wale wanaochagua kutoa kazi chache lakini zenye ubora wa hali ya juu. Kwa muktadha huo, Alikiba anaonekana kusimama katika kundi la wasanii wanaoamini katika ubora kuliko wingi.
Kwa muda mrefu sasa, Kiba amekuwa akijulikana kwa mtindo wake wa utoaji wa muziki usio wa haraka, lakini unaolenga ubora wa juu na maisha marefu ya kazi zake sokoni. Hii ni tofauti na mwenendo wa sasa wa tasnia ya muziki wa kidigitali ambapo baadhi ya wasanii huchagua kutoa nyimbo mfululizo ili kubaki juu ya chati na kwenye algorithms za streaming platforms.
Kauli yake pia imekuja katika kipindi ambacho wimbo wake mpya Finale, aliomshirikisha Bien, unaendelea kufanya vizuri kwenye majukwaa ya kidigitali. Video ya wimbo huo imekuwa ikipata watazamaji wengi na maoni chanya kutoka kwa mashabiki wa Afrika Mashariki na kwingineko, hali inayoongeza uzito wa ujumbe wake kuwa kazi moja bora inaweza kuwa na athari kubwa kuliko nyingi zisizo na nguvu sawa.
Baadhi ya wachanganuzi wanasema kijembe hicho kimemlenga mpinzani wake wa karibu Diamond Platnumz ambaye ameachia nyimbo mbili (Happy na Joy) kwenye kipindi kifupi ambacho King Kiba kaachia wimbo mmoja unaofanya vizuri zaidi ya nyimbo za Simba.
Hata hivyo, mjadala unaoibuliwa na kauli hiyo una pande mbili. Wapo wanaounga mkono msimamo wa Kiba wakisema ubora ndiyo unaojenga legacy ya msanii. Lakini pia wapo wanaoamini kuwa katika ushindani wa sasa, consistency ya kutoa nyimbo mara kwa mara ni muhimu ili kubaki relevant kwenye soko lenye ushindani mkubwa.
Kwa mtazamo wa kina, kauli ya Alikiba si tu maneno ya jukwaani bali ni tafakari ya mkakati wake wa muziki na namna anavyoiona tasnia kwa ujumla. Inaibua swali muhimu kwa wasanii na mashabiki piaāje, thamani ya msanii ipo kwenye wingi wa kazi anazotoa, au kwenye ubora na uimara wa kazi chache anazoachia?
Hadi sasa, jambo moja liko waziākauli hiyo imefanikiwa kuamsha mjadala mkubwa, na kwa mtindo wa King Kiba, huenda hata hilo lenyewe ni sehemu ya mchezo wake wa kisanii.
