Entertainment
Diddy Apatikana Bila Hatia Katika Mashtaka Mazito, Lakini Asalia Gerezani

Jopo la majaji 12 mjini New York limempata msanii maarufu wa muziki wa hip hop, Sean “Diddy” Combs, bila hatia katika mashtaka mazito yaliyomkabili, ambayo yangeweza kumpeleka kifungoni maisha.
Hata hivyo, Combs hataachiwa huru mara moja, baada ya jaji kukataa ombi lake la dhamana – na bado anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 20 jela kufuatia kutiwa hatiani kwa makosa mawili ya kusafirisha watu kwa ajili ya ukahaba.
Wataalamu kadhaa wa sheria wanasema huenda asitumikie kifungo hicho chote.
Jaji alitaja kukiri kwa upande wa utetezi kwamba Combs alijihusisha na ukatili wa majumbani katika mahusiano yake ya karibu kama sababu kuu ya kukataa ombi la dhamana.
Ingawa aliachiliwa huru kwenye mashtaka mazito zaidi, kesi hiyo ilijaa ushahidi uliotolewa na wapenzi wa zamani waliotoa maelezo ya kina kuhusu manyanyaso ya kimwili na ukatili wa majumbani.
Mawakili wa Combs walikubali kuwa alikuwa mkatili katika mahusiano yake, lakini walikanusha kuwa hilo linathibitisha kwamba alikuwa anaendesha mtandao wa kihalifu wa usafirishaji watu kwa ajili ya ngono.
Combs, ambaye amekuwa gerezani Brooklyn tangu Septemba mwaka jana, atasalia huko hadi tarehe ya kusikilizwa kwa hukumu yake tarehe 3 Oktoba.
Kesi hii imevutia umakini mkubwa. Diddy ni mmoja wa wasanii mashuhuri wa hip hop nchini Marekani, na hakuwa ameonesha dalili zozote za kustaafu kabla ya kukamatwa kwake. Kwa sasa, mustakabali wake wa karibu – pamoja na urithi wake katika muziki wa rap – bado haujajulikana.
Entertainment
Sijakataa Kuchangiwa, Ila Nipewe Heshima, Nyevu Fondo Afunguka

Muunda maudhui maarufu Pwani, Nyevu Fondo, amefunguka sababu zake za kukataa pesa za mchango wa matibabu zilizochangishwa na Presenter Jakki.
Presenter Jakki, bila kumjulisha Nyevu, alianzisha kampeni ya mchango wa matibabu kwa jina lake baada ya kujua Nyevu anaugua, akiwahamasisha mashabiki na wafuasi wake kutuma msaada wa fedha akishiriki picha za Nyevu Fondo kwenye mitandao ya kijamii.
Akizungumza hewani kwenye kipindi cha Janjaruka 254, Nyevu alisema wazi kuwa hana tatizo na watu kumchangia, lakini alikerwa na jinsi jambo hilo lilivyofanywa bila ushauriano:
“Mimi sijakataa kuchangiwa. Ni kitu poa. Kitu ambacho kinaniumiza ni kuwa kwa nini hakuniuliza mimi mwenyewe, naugua nini na nahitaji msaada aina gani? Je, ule ugonjwa unahitaji msaada wa aina gani ama kile kitu nachougua kinahitaji msaada ama ala?”
Awali kwenye ukurasa wake wa Facebook Nyevu Fondo aliandika;
Hata hivyo Presenter Jakki hajanyamaza. Kupitia mitandao yake ya kijamii, Jakki amejibu kwa hisia nzito, akieleza kusikitishwa na jinsi nia yake njema ilivyotafsiriwa vibaya mbele ya umma.
Hapa chini ni kauli yake kamili:
“Binadamu mbona tuna roho nyepesi kama korosho? 😢 Kwa nini mnanitengenezea taswira mbaya mbele ya hadhira yangu, ilhali nia yangu ilikuwa njema? Sitaki sifa wala umaarufu—nilitaka kusaidia kwa moyo wa huruma. Kumbukeni, kuna leo na kesho… na mitandao haitasahau kamwe. INTERNET NEVER FORGETS.”
“Kwa kuwa Nyevu Fondo hajaweza kupokea mchango huu, nimeamua pesa hizi nizielekeze kwenye kituo cha watoto yatima (Children’s Home) zikawe baraka kwa wengine. Labda Mungu ataniona na kunibariki. Kwa yote, nawaombea baraka – watu wa Mungu tuchukuliane kwa upendo.”
Awali Nyevu aliandika
Entertainment
Penzi Lao Lazaa Matunda: Jux na Priscilla Watarajia Mwana

Binti wa mwigizaji mashuhuri wa Nollywood, Iyabo Ojo, ambaye ni Priscilla Ojo, na mumewe, nyota wa muziki kutoka Tanzania Juma Jux, wametangaza kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza.
Wapenzi hao walishiriki habari hizo njema kupitia mtandao wa Instagram kwa picha maridadi za ujauzito, ambapo Priscilla alionekana akionyesha tumbo lake la ujauzito. Picha hizo zilifuatana na maandishi mafupi: “Mum & Dad.”
Safari ya kimapenzi ya wawili hao imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu, ikijumuisha harusi kadhaa zilizofanyika nchini Nigeria na Tanzania, hatua ambayo iliangazia muunganiko wa tamaduni zao mbili.
Juma Jux alimvisha pete ya uchumba Priscilla mara mbili, ambapo ombi la pili lilikuwa la kipekee na lisilosahaulika, lililofanyika jijini Lagos, Nigeria.
Wapenzi hao waliadhimisha safari yao ya ndoa kwa sherehe mbalimbali, zikiwemo harusi ya kitamaduni ya Kiyoruba, harusi ya kanisani (white wedding), na sherehe nyingine zilizoandaliwa kwa fahari kubwa mnamo Aprili 17 na 19, zote zikiwa jijini Lagos.
Kadiri wanavyojiandaa kwa ujio wa mtoto wao wa kwanza, pongezi na salamu za heri kutoka kwa mashabiki na jamaa zimekuwa zikitiririka kwa wingi.