Sports
Cherotich Amshinda Tena Yavi Mbio Za Oslo.

Riadha
Mkenya Faith Cherotich kwa mara nyingine tena ameweza kumshindabingwa wa Olimpiki mbio za mitaa 3000 kuruka maji na viunzi Winfried Yavi raia wa Bahrain kwa kutumia muda wake bora wa dakika 9:02.60 huku bingwa huyo wa olimpiki akimaliza nafasi ya pili kwa na dakika 9;02;76 naye Marwa Bouzayani wa Tunisia kwa muda dakika 9:06.84.
Hii ni mara ya pili kwa chipukizi huyo kubwaga Yavi ambaye makao yake ni Kenya japo anakimbilia taifa hilo la Bahrain baada ya kufanya hivyo tena msururu wa Doha Qatar mwezi jana.
Katika mbio za mitaa 800 mkenya Emmanuel Wanyonyi aliandikisha muda wake bora wa dakika 1;42.78 na kumaliza wa kwanza mbele ya Mohammed Attaoui wa Uhispania na Djamel Sedjati wa Aljeria waliotumia muda za 1;42.90 na 1;43.96 na kumaliza wa pili na tatu mtawalia.
Sports
Manchester United Ndiyo mabingwa wa ‘PREMIERE LEAGUE SUMMER SERIES’

Sports
Stars yaanza vema CHAN kwa ushindi goli 1-0 dhidi ya DR-Congo
