Sports
Chelsea Yathibitisha Kunasa Joao Pedro

Kilabu ya Chelsea imethibitisha kumsajili mshambulizi wa kilabu ya Brighton and Hove Albion FC Joao Pedro raia wa Brazil kwa pauni milioni 60.
Mchezaji huyo amesafiri tayari Marekani baada ya kukamilisha vipimo vya kimatibabu mjini london NA kutia wino mkataba wa miaka mitano na The Blues.
Nyota huyo anakua sajili wa tatu kwa Chelsea ambao mpaka sasa wametumia zaidi ya pauni milioni 200 katika kusajili wachezaji.
Pedro mwenye umri wa miaka 23 sasa yuko njia nyeupe kuwakilisha The Blues kwenye mechi ya robo fainali Kombe la Dunia baina ya vilabu nchini Marekani dhidi ya Fluminese ya Brazil.
Sports
Makocha Saba pekee Wameshinda Taji La CHAN

CHAN COUNT DOWN 16 Days to Go
Sports
Matumaini Ya United Kupata Mbeumo Yanazidi Kudidimia

Matumaini ya kilabu ya manchester united kupata huduma za kiungo mshambulizi wa kilabu ya Brenford Bryan Mbeumo yanaonekana kufifia kila kuchao.
Haya yanajiri baada ya mazungumzo hayo kukwama kwa sasa baada ya kilabu hiyo ya London kuongeza ada ya malipo ya mchezaji huyo hadi pauni milioni 70.
Kilabu ya Manchester United haiko tayari kulipa zaidi ya pauni milioni 65 kwa mvamizi huyo raia wa Cameroon.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alifunga magoli 20 ligi ya epl msimu jana.