Sports
Chelsea Mabingwa Kilabu Bingwa Duniani

Miamba wa Uingereza kilabu ya Chelsea ndiyo mabingwa wa Fainali ya Kombe la Dunia baina ya vilabu baada ya kutia darasi kabila ya kukalifisha PSG kibano cha magoli 3-0 ugani Metlife jana usiku.
Kiungo mshambulizi Cole Palmer alikua nyota wa mchezo akianza safari ya kuwapa raha mashabiki wa The Blues dakika ya 22 kabila ya kuongeza la pili dakika ya 30 kisha Joao Pedro akifunga la tatu dakika ya 43.
Kilabu ya PSG ilimaliza mechi hiyo wachezaji 10 uwanjani baada ya kiungo wa Ureno Joao Neves kulisha kadi nyekundu dakika za jioni kipindi cha Pili.
Kwa mujibu wa kocha wa Chelsea Enzo Maresca walistahili ushindi kwani walikua timu bora uwanjani huku wakilimbisha sakafu timu yenye uwezo mkubwa Psg.
“Kuanzia Mwanzo tulikua timu bora,iliounda nafasi nyingi ,timu iliyo na kiu ya ushindi tulishinda wenzetu kila sehemu uwanjani.”
The Blues sasa watakua wanapumzika kabila kuanza kuwazia ligi kuu Uingereza mwezi ujao.
Sports
Harambee Stars Kundi La Kifo Kundi B.

Sports
Kiungo Wa Brenford Bryan Mbeumo Sasa Ni Mali Ya United

Baada ya vute ni kuvute ambayo imedumu kwa kipindi cha mwezi mmoja ni rasmi kwamba kilabu ya manchester United na Brenford wameafikia makubaliano ya pauni milioni 70 ya kiungo mshambulizi Bryan Mbeumo raia wa Cameroon.
Haya yanajiri baada ya ofa mara mbili ya united kukataliwa na kilabu hio kabila ya kutuma ofa ya mwisho ya pauni milioni 65 na nyongesa ya pauni milioni 5.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 yuko tayari kumwaga wino mkataba wa miaka mitano baada kukubali matakwa yake binafsi.
Mbeumo anakua sajili wa pili kwa kocha mkuu Ruben Amorim baada ya ujio wa mshmabulizi Matheus Cunha.