Rais William Ruto amesema kuwa uchumi wa taifa umeimarika hata zaidi tangu alipoingia mamlakani.
Akizungumza na vyombo vya habari rais Ruto alidokeza kuwa mwaka wa 2022 Kenya ilikabiliwa na matatizo ya kiuchumi, huku mfumuko wa bei za bidhaa ukifika aslimia 9.6.
Kiongozi wa taifa alidokeza kuwa shilingi ya kenya ilibadilishwa kwa dola ya Marekani kwa shilingi 165 wakati huo.
Kuhusu kilimo rais Ruto alisema kumenakiliwa ongezeko la mavuno ya mahindi kutoka magunia milioni 40 mwaka wa 2022 hadi magunia milioni 64 mwaka jana 2024.
Aidha Ruto aliongeza kuwa utengezaji wa sukari umeongezeka hadi tani elfu 815.
Wakati huo huo Ruto alisema kuwa kupitia ujenzi wa nyumba za bei nafuu, nafasi za ajira zimepatikana huku serikali ikilenga kuajiri vijana milioni moja kufikia mwaka ujao 2026.
Taarifa ya Pauline Mwango