Connect with us

Sports

Gyokeres Sasa Ni Mali Ya Arsenal

Published

on

Klabu ya Arsenal imefikia makubaliano na Sporting Lisbon juu ya kumsajili mshambuliaji Victor Gyokeres kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 63.5 na nyongeza ya milioni 10.

Gyökeres, 27, raia wa Sweden anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano utakaombakisha kwa Washika Mitutu hao mpaka Juni 2030.
Kumekuwepo na sintofahamu kuhusiana na uhamisho huo baada ya Kilabu ya Manchester United kujaribu kupokonya Arsenal Mshambulizi huyo Ila Mshambulizi huyo alisalia kwamba anataka Arsenal pekee.
Mchezaji huyo anakua sajili wa tano kwa The Gunners baada ya usajili wa kipa Kepa Arrizabalaga,kiungo Martin Zubimendi,Christian Norgard na Mosquera.
Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Sports

Tanzania Kupitia Wizara Ya Michezo Yaanza Hamasa Kwa Mashabiki Kuelekea Chan

Published

on

By

Hamasa za mashabiki wa Taifa Stars kuelekea michuano ya CHAN 2024 itakayoanza Agosti 2,2025 rasmi zimezinduliwa leo Julai 22,2025 viwanja vya Mbagala Zakhem.
Taifa la Tanzania kupitia kwa Wizara ya michezo hii leo imeanzisha hamasa za michuano ya Chan ambayo inangoa nanga Agosti 2 ugani Benjamin Mkapa nchini Humu.
Shughuli hiyo kulingana na Waziri msaidizi wa wizara ya Michezo Hamis Mwinjuma ni sehemu ya kurai mashabiki kujitokeza kwa wingi kutazama michuano hiyo na kushabikia vijana wa nyumbani timu ya Taifa Stars.
Taifa hilo linafungua kampeini yake dhidi ya Burkina Faso mechi za kundi B kabila ya kukwaruzana na Mauritania,kisha Madagascar kabila ya kufunga na Central Afrika Republic.
Continue Reading

Sports

Chipolpolo Ya Zambia Inazidi Kujinoa Kambini Lusaka Tayari Kwa Chan

Published

on

By

SIKU 11 ZIMESALIA KWA KOMBE LA CHAN KUNGOA NANGA

ZAMBIA- Chipolopolo

Hii leo tunangazia Taifa la Zambia,wanajiita Chipolopolo kwa jina la Utani,ikiwa inaorodheshwa nafasi ya 87 kote ulimwenguni na Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA.

Kocha mkuu wa Kikosi hicho ni Avram Grant raia wa taifa la Israel, hata hivyo kwenye kipute cha Chan vijana hao wataongozwa na kocha wa nyumbani na mshambulizi wa zamani wa Nchanga Rangers na Power Dynamos Wedson Nyirenda.

Chipolopolo wameshiriki kombe hilo mara nne (2009, 2016, 2018, 2020) ila wameambulia patupu bila kushinda wakimaliza ya tatu katika mwaka wa kwanza wa kombe hilo mwaka 2009 nchini DR.Congo.

Timu hiyo ni mabingwa mara moja taji la AFCON wakishinda mwaka 2012 na pia ni mabingwa mara saba kombe la COSAFA ukanda wa Afrika Kusini.

Timu hiyo yenye wachezaji 32 itaongozwa na nahodha na mzee wa kazi beki wa zamani wa TP Mazembe  Kabaso Chongo ambaye kwa sasa anapiga na Kabwe Worriors ya taifa hilo.

Badhi ya nyota wengine wa kuangaziwa katika kikosi hicho ni pamoja na mshambulizi Joseph Phiri na Evans Kayombo;

GOALKEEPERS); Francis Mwansa (Zanaco), Willard Mwanza (Power Dynamos), Levison Banda (Zesco United), Charles Kalumba (Red Arrows).

(DEFENDERS); Benedict Chepeshi, Kabaso Chongo (all Zesco United), Mathews Banda, Kendrick Mumba, (both Nkana), Killian Kanguluma (Kabwe Warriors), Kebson Kamanga, Happy Nsiku (all Red Arrows), Lyson Banda (Green Buffaloes), Dominic Chanda (Power Dynamos), John Chishimba (Zanaco).

(MIDFIELDERS); Owen Tembo, Frederick Mulambia, Prince Mumba (both Power Dynamos), Kelvin Kapumbu (Konkola Blades), Wilson Chisala (both Zanaco), Philimon Chilimina (both Green Buffaloes), Rally Bwalya (Napsa Stars), Abraham Siankombo, Kelvin Kampamba (both Zesco United), Jackson Kampamba (Mutondo Stars), Kenneth Kasanga (Nkwazi), Timothy Sichalwe (Athletico), Kelvin Mwanza (Muza FC).

(STRIKERS); Andrew Phiri (MUZA), Evans Kayombo (Napsa Stars), Charles Zulu (Nkana), Joseph Phiri (Red Arrows), Kenan Phiri (Makeni All Stars).

Zambia wako kundi A pamoja na Kenya,Angola,Morocco na Dr. Congo

Continue Reading

Trending