Connect with us

Sports

Arsenal Mbioni Kumpata Mshambulizi Sesko

Published

on

Kilabu ya Arsenal imeambiwa ni lazima itoe kitita cha pauni milioni 75 kunasa huduma za mshambulizi wa taifa la Slovenia na kilabu ya RB Leipzig Benjamin Sesko.

Inaaminika na The Gunners kupitia kwa Afisa mkuu mtendaji Andrea Berta wamekua na mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa mchezaji huyo na pia afisa wa Leipzig Marcel Schafer kuhusiana matakwa ya uhamisho huo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alikua na magoli 21 msimu huu akichangia mengine sita katika michezo yote alizoshirikisha akiwa miongoni mwa wafungaji bora ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani.

The Gunners wako sokoni kusaka mshambulizi atakayewapa taji msimu ujao huku ikidaiwa pia watafanya mazungumzo na mshambulizi wa Sporting Lisbon Victor Gyokeres ambaye alifunga zaidi ya magoli 40 msimu ambao umekamilika.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Sports

INZAGI Bado Yuko Saana Inter.

Published

on

By

Uongozi wa klabu ya Inter Milan uko radhi kurefusa mkataba wa kocha Simone Inzaghi licha ya kufeli
kutwaa taji la klabu bingwa Uropa siku ya jumamosi.
Rais wa Inter Giuseppe Marotta, ameelezea Imani kwa uongozi wa Kocha Inzaghi, licha ya kibano cha
magoli 5-0 klabu hiyo ilipokea katika fainali ya klabu bingwa uropa dhidi ya Paris Saint-Germain
(PSG) na kupoteza fainali ya pili mtawalia, ya kwanza ikiwa msimu wa mwaka 2022/2023 mikononi
mwa Manchester City.
Mkataba wa Inzaghi unakamilika mwezi juni mwaka ujao ila Marotta, amesisitiza kuwa mazungumzo na
kocha huyo yataanza hivi karibuni, baada ya tetesi kuwa Inzaghi anajiondoa Inter na hatakuwepo
kuitayarisha kwa ajili ya msimu ujao.
“Kushindwa katika fainali hauna msukumo wowote, inzaghi ana mkataba wa mwaka mmoja Zaidi na
tuliamua kukutana naye juma hili” Alisema Marotta katika kikao na wanahabari baada ya fainali ya klabu
bingwa uropa huko Munich Ujerumani. “Mafanikio yote na makali ya klabu yanayoonekana ni kwa ajili
ya uwezo na utaalam wake,Tutafurahia iwapo yuko radhi kuendelea na kazi.”

Continue Reading

Sports

Inter Wapiga Msamba, PSG Wakivuma Uefa.

Published

on

By

Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ndio mabingwa wa Klabu bingwa Uropa baada ya kuilaza Inter-Milan magoli 5-0 Jumamosi usiku, katika fainali iliyochezewa katika uwanja wa Allianz Arena jijini Munich, Ujerumani.

Mvua ya magoli ilianzishwa na beki Ashram Hakimi dakika ya 12, kabla ya kiungo mshambuliaji wa PSG Desire Doue kuongeza bao la pili dakika ya 20, na goli la tatu katika dakika ya 60 huku goli la nne na tano likifungwa katika dakika ya 73 na 86 mtawalia.

Kocha wa PSG Luis Enrique amewasifia wachezaji wake sawa na mashabiki waliojitokeza kuishangilia klabu hiyo, ikijipatia taji kuu la kwanza Uropa baada ya kuingia fainali ya mashindano haya mara mbili kwa kipindi cha miaka mitano.

“Nafurahia sana ushindi huu” Alisema Kocha Enrique. “Fainali imekua na hisia sana hasa nilipoona bango la mashabiki kuhusu familia yangu”

Kikosi hichi changa cha PSG kimeafikia kile ambacho wachezaji nyota kama Lionell Messi, Neymar, Zlatan Ibrahimovich, Beckam na Kylian Mbappe walishindwa kutekeleza wakivalia jezi ya PSG

Paris Saint-Germain (PSG) imekua klabu ya pili Ufaransa kushinda taji la Klabu bingwa Uropa baada ya Marseille mwaka 1993.

Continue Reading

Trending