Sports
Wanahabari Wapokea Mafunzo ya Uandishi Siku Moja Kabla ya Kip Keino Classic

Waandishi wa habari kutoka Kenya wamepokea mafunzo ya kiufundi kuhusu namna ya kuripoti mashindano ya riadha ya hadhi ya kimataifa, yakiwemo ya toleo la sita la Absa Kip Keino Classic Continental Tour, yatakayofanyika katika Ulinzi Sports Complex.
Afisa Mawasiliano wa Riadha za Dunia, Antonio Carvalho, aliongoza warsha hiyo Alhamisi, Mei 29 na kuwapa wanahabari mbinu muhimu za kuripoti, hasa kwenye eneo la mahojiano ya haraka (flash interviews).
“Katika kunukuu wanariadha, zingatia maneno yanayoonesha utu wao, yanayoeleza ni nini kinachowafanya kuwa wa kipekee, na yanayobeba simulizi ya kipekee kuhusu mhusika,” alisema Carvalho.
Carvalho pia alisisitiza umuhimu wa waandishi kufanya utafiti wa awali kuhusu historia ya wanariadha kabla ya kuripoti mashindano ya kiwango cha juu kama Kip Keino Classic.
“Tovuti ya World Athletics (www.worldathletics.org) ni rasilimali muhimu. Ina taarifa nyingi kuanzia wasifu wa wanariadha, orodha za kuanza mashindano, hadi matokeo ya awali,” alieleza.
Aliongeza kuwa waandishi wa habari wanapaswa kufahamu maswali ya kuuliza ili kupata nukuu bora kutoka kwa wanariadha, na pia kuwa makini katika kufuatilia matokeo ya mashindano pamoja na hali ya mazingira wakati mashindano yanaendelea.
Katika warsha hiyo, Carvalho alisisitiza kuwa waandishi wa habari wanaoshughulika na flash quotes wanapaswa kuelewa kwa kina mienendo ya mchezo wa riadha ili kutoa taarifa bora na sahihi.
Pia, warsha hiyo ilitoa elimu muhimu kuhusu masuala ya Dhulma za Kijinsia (GBV) ambazo zimeathiri tasnia ya michezo, ikiwemo visa vinavyohusiana na Agnes Tirop wa Kenya na Rebecca Cheptegei wa Uganda.
Kikao hicho cha maingiliano kiliongozwa na Chris Mbaisi, Rais wa zamani wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Kenya (SJAK).
Rais wa sasa wa SJAK, James Waindi, aliwashukuru waandaaji wa warsha hiyo kwa juhudi zao na kuhimiza kuandaliwa kwa warsha zaidi zinazolenga kuwaunganisha wanahabari na wadau wa michezo.
Mashindano ya Kip Keino Classic ni moja ya mashindano ya siku moja ya kiwango cha juu duniani, yakiwa sehemu ya mashindano ya Continental Tour Gold Series ya Shirikisho la Riadha Duniani.
Toleo la mwaka huu linalotarajiwa kufanyika Jumamosi, Mei 31 kwenye Uwanja wa Ulinzi litawavutia wanariadha mashuhuri kutoka Afrika na mabara mengine, hivyo kuwapa wanariadha wa Kenya nafasi ya kushindana katika kiwango cha kimataifa.
Washiriki wa mashindano hayo watapigania zawadi ya fedha pamoja na pointi muhimu kwa viwango vya ubora vya dunia (world ranking points).
Sports
Mancity Inamnyemelea Kiungo Tijjani Reijnders

Kilabu ya Manchseter City iko kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na kiungo wa AC Milani Tijjani Reijnders kumleta ugani Etihad msimu ujao.
Mawakala wa mchezaji huyo wanataka kitita cha pauni milioni 60 kumwachilia mholanzi huyo ambaye amefunga magoli 19 katika mechi 104 ambazo amechezea Milan
Hata hivyo city wako tayari kutoa pauni milioni 55 kupata sahihi yake na kumpa kandarasi nono mkataba wa miaka mitano ugani Etihad.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Milan msimu jana akitokea AZ Alkamar ya Eredivise.
City wangali sokoni kupata mrithi wa kiungo mbunifu Kevin De Bruyne ambaye ameondoka kwenye kilabu hiyo baada ya mafanikio makubwa ikidaiwa pia wanamfukuzia kiungo wa Lyon Ryan Cherki raia wa Ufaransa.
Sports
Arsenal Mbioni Kumpata Mshambulizi Sesko

Kilabu ya Arsenal imeambiwa ni lazima itoe kitita cha pauni milioni 75 kunasa huduma za mshambulizi wa taifa la Slovenia na kilabu ya RB Leipzig Benjamin Sesko.
Inaaminika na The Gunners kupitia kwa Afisa mkuu mtendaji Andrea Berta wamekua na mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa mchezaji huyo na pia afisa wa Leipzig Marcel Schafer kuhusiana matakwa ya uhamisho huo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alikua na magoli 21 msimu huu akichangia mengine sita katika michezo yote alizoshirikisha akiwa miongoni mwa wafungaji bora ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani.
The Gunners wako sokoni kusaka mshambulizi atakayewapa taji msimu ujao huku ikidaiwa pia watafanya mazungumzo na mshambulizi wa Sporting Lisbon Victor Gyokeres ambaye alifunga zaidi ya magoli 40 msimu ambao umekamilika.