Connect with us

News

WAVUVI MJINI KILIFI HAWANA VIFAA VYA KISASA VYA UVUVI

Published

on

Mwenyekiti wa wa wahudumu wa maboti Kilifi mjini kaunti ya Kilifi, Shallo Issa maarufu captain Shallo amesisitiza haja ya wavuvi wa eneo hili kuimarishwa kupitia vifaa vya kisasa vya uvuvi.

Akizungumza na Coco Fm, Shallo amesema kuwa wavuvi wengi wanashindwa kwenda kuvua kwenye maji makuu kutokana na ukosefu wa boti za kisasa sawa na nyavu na mishipi ya kisasa.

Licha ya kuwa mradi wa maendeleo ya jamii, kiuchumi na uvuvi KEMFSED uliwasaidia kwa kuwapata baadhi boti, Shallo amesema bado boti hizo ni ndogo mno na haziwezi kuhimili mawimbi kwenye maji makuu jambo linalopelekea shinikizo zao za kuitaka serikali kuwaimarisha kwa vifaa Zaidi vya kisasa.

Kufuatia hilo Shallo amesema kuwa wavuvi wengi wanaendelea kuathirika kutokana na wao kushindwa kuvua samaki kwa wingi ikizingatiwa kwamba samaki wengi hupatikana kwenye maji makuu.

 

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Kilabu Ya Liverpool Yamnasa Frimpong

Published

on

By

Beki wa kilabu ya Bayern Leverkusen Jeremie Frimpong ni rasmi amejiunga na mabingwa wa ligi kuu Uingereza Liverpool.

Beki huyo mholanzi amejiunga na The Reds kwa pauni milioni 29.5 na amemwaga wino mkataba wa miaka 5 na kilabu hio kuchukua nafasi ya Alexander Trent Arnaold ambaye ni rasmi amejiunga na kilabu ya Real Madrid.

Mholanzi huyo anakua mchezaji wa tano kuvalia jezi ya kilabu hio wengine akiwa ni pamoja na Cody Gakpo,Virgil Van Dijik,Ryan Gravenberch.

Nyota huyo ambaye pia amekuwa akiwindwa na Manchester United na miamba wa Uhispania Rea Madrid amesema kwamba alichagua kilabu hiyo kwani ndio inaendana na mipango yake ya mbeleni kama mchezaji akiahidi kushinda mataji na miamba hao wa Uingereza.

Continue Reading

News

Shughuli za Masomo Zatatizwa katika Shule ya Msingi ya Arabuko Sokoke

Published

on

By

Shughuli za masomo katika shule ya msingi ya Arabuko Sokoke eneo la Kakuyuni kaunti ya Kilifi zilitatizika mapema siku ya Ijumaa baada ya Wazazi kuandamana wakilalamikia usimamizi mbaya wa shule hiyo.

Wakaazi hao wamemtaka Mwalimu kuu wa shule hiyo kupewa uhamisho kwani ameonyesha wazi kushindwa kusimamia shughuli za masomo katika shule hiyo.

Wakiongozwa na Joyce Mbuche, Wazazi hao wamesema Mwalimu mkuu wa shule hiyo amekosa kuwa wazi kwa wazazi kuhusu suala la matumizi ya Fedha ya shule hiyo pamoja na kutokuwa muadilifu kazini.

Wazazi hao hata hivyo wamesema Mwalimu mkuu huyo amekuwa hawalipi mishahara walimu ambao wanasimamiwa na wazazi katika shule hiyo huku baadhi ya wanafunzi wakikosa kusajiliwa katika mfumo wa KEMIS.

Continue Reading

Trending