News
Mahakama ya Kilifi Imeagiza Kuzuiliwa Rumande Mshukiwa wa Unajisi

Mahakama ya Kilifi imeagiza kuzuiliwa rumande kwa mshukiwa wa unajisi wa mtoto umri wa miaka 7 wakati kesi hiyo ikiendelea.
Hakimu Mkuu wa Mahakama hiyo Ivy Wasike ametoa agizo hilo akisema mshukiwa huyo anafaa kurudishwa Mahakamani mnamo tarehe 29 mwezi Mei mwaka huu.
Kabla ya agizo hilo, Mahakama imeelezwa kwamba mnamo tarehe 6 mwezi Februari mwaka huu mshukiwa Julius Mramba alitekeleza kitendo hicho katika maeneo ya Matsangoni kaunti ya Kilifi.
Mahakama pia imeelezwa kwamba mshukiwa alitekeleza unyama huo baada ya kuandamana na mtoto huyo hadi shambani kuchukua Nazi alizokuwa ameagizwa na mama wa mtoto huyo.
News
Kilabu Ya Liverpool Yamnasa Frimpong

Beki wa kilabu ya Bayern Leverkusen Jeremie Frimpong ni rasmi amejiunga na mabingwa wa ligi kuu Uingereza Liverpool.
Beki huyo mholanzi amejiunga na The Reds kwa pauni milioni 29.5 na amemwaga wino mkataba wa miaka 5 na kilabu hio kuchukua nafasi ya Alexander Trent Arnaold ambaye ni rasmi amejiunga na kilabu ya Real Madrid.
Mholanzi huyo anakua mchezaji wa tano kuvalia jezi ya kilabu hio wengine akiwa ni pamoja na Cody Gakpo,Virgil Van Dijik,Ryan Gravenberch.
Nyota huyo ambaye pia amekuwa akiwindwa na Manchester United na miamba wa Uhispania Rea Madrid amesema kwamba alichagua kilabu hiyo kwani ndio inaendana na mipango yake ya mbeleni kama mchezaji akiahidi kushinda mataji na miamba hao wa Uingereza.
News
Shughuli za Masomo Zatatizwa katika Shule ya Msingi ya Arabuko Sokoke

Shughuli za masomo katika shule ya msingi ya Arabuko Sokoke eneo la Kakuyuni kaunti ya Kilifi zilitatizika mapema siku ya Ijumaa baada ya Wazazi kuandamana wakilalamikia usimamizi mbaya wa shule hiyo.
Wakaazi hao wamemtaka Mwalimu kuu wa shule hiyo kupewa uhamisho kwani ameonyesha wazi kushindwa kusimamia shughuli za masomo katika shule hiyo.
Wakiongozwa na Joyce Mbuche, Wazazi hao wamesema Mwalimu mkuu wa shule hiyo amekosa kuwa wazi kwa wazazi kuhusu suala la matumizi ya Fedha ya shule hiyo pamoja na kutokuwa muadilifu kazini.
Wazazi hao hata hivyo wamesema Mwalimu mkuu huyo amekuwa hawalipi mishahara walimu ambao wanasimamiwa na wazazi katika shule hiyo huku baadhi ya wanafunzi wakikosa kusajiliwa katika mfumo wa KEMIS.