News
Papa Leo XIV Achangulia Rasmi

Kadinali Robert Francis Prevost kutoka taifa la Marekani ndiye Papa mpya aliyechaguliwa kuongoza Kanisa Katoliki kote duniani.
Kadinali Prevost amechagua jina la Papa Leo XIV.
Papa Leo XIV ana umri wa miaka 69 na alizaliwa Septemba 14 mwaka wa 1955 na ana uraia wa taifa la Peru na Marekani.
Hatua hiyo, ameafikiwa baada ya Makadinali kutekeleza jukumu lao la kitume la kupigia kura Kiongozi ambaye atachukua jukumu la kuongoza Kanisa Katoliki kote duniani.
Makadinali 133 walikuwa wakiendeleza mchakato wa kumchagua Papa mpya katika kipindi cha siku mbili katika Kanisa la Sistine mjini Vatican na hatimaye kuafikia kumpata Papa Leo XIV ambaye ataongoza waumini wa Kanisa Katoliki.
Papa Leo XIV, anatarajiwa kuhakikisha anaendeleza mshikamano wa waumini na amani kote ulimwenguni ikiwemo kutafuta mwafaka wa mizozo ya vita katika mataifa mbalimbali.
Papa Leo XIV atakuwa Papa wa 267.
News
Kesi dhidi ya Mackenzie na washukiwa wenzake 38 inaendelea Mahakamani

Kesi dhidi ya mhubiri tata Paul Mackenzie na washukiwa wenzake 38 kuhusu ukatili na ukiukaji wa haki za watoto inaendelea kusikizwa katika mahakama ya watoto ya Tononoka kaunti ya Mombasa mbele ya hakimu mkuu Nelly Chepchirchir, mashahidi 3 wakishuhudia.
Shahidi wa 47 ambaye ni mtaalamu wa tiba ya watoto kutoka kituo cha watoto cha Malindi kaunti ya Kilifi, ameeleza mahakama hali dhaifu ya kisaikolojia ya mvulana mdogo aliyekuwa miongoni mwa watoto 8 waliookolewa kutoka kwenye msitu wa Shakahola.
Amesema mazungumzo ya usaidizi na uchunguzi wa kitabibu yaliwasaidia watoto kukabiliana na msongo wa mawazo.
Mtaalamu huyo amesema pia baada ya tathmini yake ya kitaalamu, alipendekeza mazingira salama ya malezi ya msaada kwa mtoto huyo kwasababu alikuwa na hofu ya kurudishwa Shakahola.
Pia amehitaji msaada wa kisaikolojia wa mara kwa mara kwa sababu alikuwa na wasiwasi kuhusu familia yake waliopotea.
Naye shashidi wa 48 na 49 Zadock Odiaho na mkewe Deborah wameeleza jinsi mwanao Wilfred Mulama na mkewe walivyowatoa watoto wao wawili shuleni na kujaribu kuwashawishi watoto wa majirani kuwa kwenda shule ni dhambi.
Wameiambia Mahakama kwamba baadae Mulama alikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja cha uangalizi kwa kushindwa kuwapeleka watoto shule akiwa na wajibu wa kuripoti kwa polisi kila wiki lakini kabla ya kifungo hicho kukamilika, alitorokea Shakahola na familia yake yote.
Wameeleleza Mahakama kwamba Mulama aliuza vitu vyake vyote kabla ya kutoweka na kuhamia Shakahola.
Wameiambia Mahakama kuwa waliwahi kuwasiliana na wachunguzi wa kesi za Shakahola, waliomwambia kuwa walikuwa wameokoa mjukuu wake msituni baada ya kupigwa hadi kushindwa kutembea.
News
Washukiwa wa uhalifu wakamatwa maeneo ya Likoni kaunti ya Mombasa

Mafisa kutoka kituo cha polisi cha Vijiweni eneo la Likoni kaunti ya Mombasa, usiku wa kuamkia leo wamewakamata wanaume watatu wanaoshukiwa kuwa wahalifu katika maeneo ya Likoni na sehemu za Kaunti ya Kwale.
Kulingana na ripoti za polisi, watuhumiwa hao, Abubakar Juma Koba mwenye umri wa miaka 17, Ali Bakari mwenye umri wa miaka 17 na Mohamed Ruwa mwenye umri wa miaka 18 ni wanachama wa kundi la vijana wanaotumia mapanga, ambao wanashutumiwa kwa kuwahangaisha wakazi katika maeneo ya Mwaweche Magulani na Dongo Kundu.
Watuhumiwa walikamatwa wakati wa doria ya usiku kufuatia taarifa za kijasusi.
Wengine watano walifanikiwa kutoroka.