News
Waziri Murkomen kutathmni hali ya usalama kwenye kaunti za Meru, Embu na Tharaka Nithi

Waziri wa Usalama wa ndani Kipchumba Murkomen, anazuru kaunti za Meru, Tharaka Nithi, na Embu, kutathmini hali ya usalama.

Waziri Kipchumba Murkomen akiwa kaunti ya Meru/picha kwa hisani
Murkomen ambaye kwa sasa y uko kwenye kaunti ya Meru, atashiriki mkutano na kamati ya usalama ya Meru, kabla ya kuzuru kituo cha usajili wa vitambulisho na kampeni dhidi ya mihadarati inayoongozwa na mamlaka ya kukabiliana na pombe na dawa za kulevya (NACADA).
Aidha, Murkomen atashiriki misururu ya mikutano na wananchi katika uwanja wa michezo wa Kinoru kuhusu maswala ya usalama.
Mikutano ya Jukwaa la Usalama uhudhuriwa na maafisa wa serikali ya taifa kuanzia kwa kamishna wa kaunti hadi kwa naibu wa chifu, viongozi wa jamii, wafanyabiashara na vijana.
Katika kaunti ya Meru, Murkomen ataangazia upya swala la wizi wa mifugo katika mpaka wa Meru na Isiolo.
Kaunti ya Meru pia inakabiliwa na mizozo ya muda mrefu ya ardhi, hususan katika mpaka wa Meru na Tharaka Nithi.
News
Washukiwa wa uhalifu wakamatwa maeneo ya Likoni kaunti ya Mombasa

Mafisa kutoka kituo cha polisi cha Vijiweni eneo la Likoni kaunti ya Mombasa, usiku wa kuamkia leo wamewakamata wanaume watatu wanaoshukiwa kuwa wahalifu katika maeneo ya Likoni na sehemu za Kaunti ya Kwale.
Kulingana na ripoti za polisi, watuhumiwa hao, Abubakar Juma Koba mwenye umri wa miaka 17, Ali Bakari mwenye umri wa miaka 17 na Mohamed Ruwa mwenye umri wa miaka 18 ni wanachama wa kundi la vijana wanaotumia mapanga, ambao wanashutumiwa kwa kuwahangaisha wakazi katika maeneo ya Mwaweche Magulani na Dongo Kundu.
Watuhumiwa walikamatwa wakati wa doria ya usiku kufuatia taarifa za kijasusi.
Wengine watano walifanikiwa kutoroka.
News
Wanaosajiliwa Kwenye Mpango wa Kazi “Majuu” Waonywa.

Waziri wa Leba nchini Dakta Alfred Mutua amewaonya vijana waliopata nafasi za ajira ughaibuni dhidi ya kujihusisha na visa vya utovu wa nidhamu.
Akizungumza wakati wa zoezi la kusajili vijana kwenye mpango wa ajira za nje nchi maarufu Kazi “Majuu” katika kaunti ya Kwale, Waziri Mutua alitaja hatua hiyo kwamba huenda ikachangia kandarasi zao kufutiliwa mbali sawa na kukabiliwa kisheria.
Mutua alidokeza kwamba kuna baadhi ya vijana ambao tayari wamerejeshwa nchini kufuatia visa vya utovu wa nidhamu
“Unaskia unawashwa unataka kuandamana, unataka kuwa mwanaharakati, unataka kuchochea ingia ndege uje hapa wikendi moja uandamane kila mahali hiyo kitu ikutoke urejee kazini, kwa sababu ukienda kufanya huko maandamano unaharibia wakenya wengine, kuna watu waliandamana huko nchi tofauti tofauti, wakenya kumi na tano wengi wakasimamishwa, wakaregeshwa nyumbani, unaandamana kwa nchi nyengine wanauliza mbona mkenya anaandamana na mganda haandamani, mbona mtanzania haandamani”, alisema waziri Mutua.
Akizungumzia suala la utumizi wa dawa za kulevya, Waziri Mutua amewataka vijana hao kukomesha uraibu huo kwani hakuna taifa linaloshabikia matumizi ya dawa za kulevya.
“Hapa utafanyia ukaguzi wa kiafya kama umekuwa ukivuta bangi, madawa ya kulevya utaanguka, hata ukikataa kupatikana hapa ukifika ng’ambo utapatikana, kwa hivyo kama unataka kwenda ng’ambo achana na bangi bwana”,aliongeza waziri Mutua.
Zoezi hilo lililenga vijana 800 kaunti ya Kwale na 3,500 eneo la pwani kwa ujumla.
Taarifa ya Joseph Jira