News
Gor Mahia Yailaumu Fkf Kutokana Na Vurugu Gusii

Mabingwa mara 21 ligi kuu humu nchini kilabu ya Gor Mahia imeilaumu shirikisho la soka nchini FKF pamoja na kamati inayosimamia ratiba ya mechi za ligi kuu kutokana na vurugu iliyoshuhudiwa ugani Gusii wikendi.
Kupitia barua kilabu hiyo imelaani kitendo hicho huku ikisema kwamba shirikisho pamoja na wasimamizi wa ligi hiyo waliwapuuza kutokana na ubora wa uwanja huo kuandaa mechi kubwaa kama hiyo ila wakapuuza kabisaa.
Kulingana na katibu mkuu wa kilabu ya Gor mahia Nicanor Arun ni kwamba hawatachezea tena uwanjani humo siku zijazo wakilaumu mashabiki wa Shabana kwamba ndio walianza vurugu hiyo ugani Gusii.
Katibu huyo aliendelea kusema alishangaa licha ya kamanda wa mechi hiyo kutaka mechi hiyo kuhairisha viongozi wa Shabana walisisitiza mechi iendelee kama ilivyopangwa.
Takwimu ambazo zimetolewa na maafisa wa usalama ni kwamba zaidi ya watu 72 waliweza kutibiwa baada ya kujeruhiwa kwenye vurumahi hio kogalo wakiponyoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya wapinzani wao Shabana.
News
Askofu Anyolo: Kadinali Njue Hatahudhuria Conclave

Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Nairobi limetangaza kwamba John Kadinali Njue, hatashiriki Kongamano la kumchagua Papa mpya wa Kanisa Katoliki duniani.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa na Kanisa hilo siku ya Jumanne, Kadinali Njue ambaye anastahili kupiga kura katika Kongamano hilo maarufu Conclave alikuwa amepokea mwaliko rasmi kutoka Shirika la kitume ili kuhudhuria Kongamano hilo ambalo linafaa kuanza rasmi tarehe 7 mwezi Mei mwaka huu lakini hataweza kusafiri.
Kanisa hilo limesema Mwakilishi wa Papa nchini Kenya Askofu Hubertus Marie Van Megen baada ya kushauriana na ofisi ya Askofu mkuu wa Nairobi Phillip Anyolo, alitoa taarifa kwamba Kadinali Njue mwenye umri wa miaka 80 hataweza kusafiri hadi Vatican- Roma kwa Kongamano hilo.
Picha kwa hisani
Askofu Anyolo amewataka waumini wa Kanisa Katoliki kuombea makadinali wanaochukua jukumu zito la kumchagua Papa mpya huku akihimiza maombi zaidi kwa ajali ya Afya na ustawi wa Kadinali Njue.
News
Wachezaji 3 Kumkaba Yamal Leo Kilabu Bingwa

Mkufunzi wa kilabu ya Inter Milan ya Italia Simeone Inzaghi amesema kwamba mechi ya leo kati yao na Fc Barcelona ni kufa kupona wakilenga tiketi ya kufuzu fainali ya kilabu bingwa ulaya mei 31 uwanjani Allianz Arena.
Akizungumza saa chache kabla ya mtanange huyo mwalimu huyo aidha amekiri ili kushinda mechi hiyo ni lazima wapate mbinu ya kuwazuia vizuri wapinzani wao kwa ustadi mkubwa la si hivyo watawadhuduru.
Miongoni mwa mikakati ambayo ameweka kocha huyo ni wachezaji watatu kumdhibiti winga matata na tineja Lamine Yamal mwenye umri wa miaka 17.
Kwa mujibu wa kocha huyo kama kuna mchezaji atasaidia Barcelona kuingia fainali basi ni makali ya mhispanyola Yamal,mchezaji huyo fundi alifunga goli kabla ya kuchangia lingine timu hizo ziktoka sare ya magoli 3-3 ugani stade olympique st.luis catalunya.
Na Simeone amesisitiza ni lazima wasimpe nafasi tineja huyo akitaka wachezaji watatu wawe naye anashika mpira.
Mechi hiyo inapigwa majira saa nne usiku Jumanne hii Ugani Sansiro Italia.