News
Mambo Atakia Kheri Rising Stars Misri Afcon u20

Kiungo wa zamani timu ya taifa ya soka Harambee Stars Robert Mambo ametakia vijana wa timu chipukizi Rising Stars kila la kheri katika mashindano ya Afcon kwa chipukizi wakianza kampeini dhidi ya Morocco Mei 1.
Akizungumza kutoka Sweeden kupitia kanda ya video Mambo ameshukuru Rising Stars kupata nafasi hiyo ya kuakilisha taifa mjini Cairo akitaka wawe na ujasiri wasiogope timu yoyote.
“Kwanza Nishukuru Vijana wa Rising Stars pamoja na kocha Salim Babu,Hii ni fursa ya stars kuonyesha makali yao kwani mechi hizi ni kama mechi zingine,msiogope yeyote kwani tuna uwezo wa kushinda mtu yeyote kombe hili.”
Kulingana na Mambo ambaye kwa sasa amechukua mafunzo ya ukufunzi nchini Sweeden ni kwamba licha ya kundi hilo kuwa ngumu Rising stars hawafai kuonekana mnyonge hata kidogo kwa sababu wako kumi 11 uwnajani kama wenzao
“Msiogope yeyote kwani mmejitayarisha vya kutosha na ni muda wa kuenjoy na kushowcase vipaji vyenu kwa dunia. ” -Mambo.
Rising Stars wako kundi B pamoja na Morocco,Tunisia na Nigeria.
News
Jopo la ushauri na Maimamu eneo la Takaungu lasisitiza Samuel Charo alisilimu kwa hiari yake

Jopo la ushauri na maimamu katika eneo la Takaungu wadi ya mnarani kaunti ya Kilifi limepinga madai yalioibuliwa na wanafamilia wa kijana aliyeuawa baada ya kumuua na kula matumbo ya mzee mmoja aliyekuwa ustadh aliyetambulika kama Ainen.
Kwa mujibu wa ustadh Abubakar Ratili wa masjid Answar kule Takaungu, marehemu Samuel Kirao Charo alisilimishwa na kupewa jina Zakariyah akisisitiza kuwa marehemu alisilimu kwa hiyari yake mbele ya waislam wengine kwenye msikiti huo
Aidha Sheikh Mahadh Ali ambaye pia ni imam wa msikiti Maryam eneo hilo la Takaungu pamoja na Ustadh Mohamed Khamis wameeleza kuwa dini ya kiislam inaruhusu mwili kuzikwa usiku akikashifu swala la kuhusisha hatua hiyo na ushirikina kama ilivyodaiwa na baadhi ya watu.
Jopo hilo pia limeeleza kuwa wanafamilia walihusishwa ila walidinda kushirikiana nao jambo lililopelekea jamii hiyo ya kiislamu kuendeleza maziko ya marehemu kwa mujibu wa Imani ya dini ya kiislam.
News
Wanaharakati na vijana wa Gen -z wazua purukushani kwenye majengo ya bunge la Mombasa
Wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu na vijana wa Gen – Z katika kaunti ya Mombasa wemezuiwa kuingia katika bunge la kaunti ya Mombasa kuwasilisha malalamishi yao kuhusiana na bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2025/26.
Vijana hao pamoja na wanaharakati hao waliojawa na hasira wanasema wenyeji wa Mombasa hawajahusishwa kiukamilifu Katika mchakato huo tofauti na inavyofanyika kwenye kaunti zingine nchini.
Wanadai hali ya kutokuwa na uwazi katika utekelezaji wa miswada ya fedha kwenye kaunti hiyo kunachangia kwa shughuli mbalimbali kaunti ya Mombasa kukosa kutekelezwa ipasavyo
Hatahivyo baadae Karani wa bunge la kaunti ya Mombasa salim Juma alipokea malalamishi yao na kuahidi kutoa mwelekeo ufaao Jumanne wiki ijao huku vijana hao wakitishia kurudi tena iwapo malalamishi yao hayatatiliwa maanani.

Bunge la kaunti ya Mombasa/Picha kwa hisani