Sports
George Foreman: Bingwa wa Masumbwi Afariki Dunia Akiwa na Miaka 76

News
Liverpool Kutangazwa Bingwa Mpya Epl

Miamba wa Uingereza kilabu ya Liverpool kutangazwa mabingwa wapya wa ligi kuu EPL Wikendi hii iwapo watatoka sare ya aina yoyote dhidi ya kilabu ya Tottenham Hotspurs ugani Anfield.
Haya yanajiri baada ya kilabu nambari mbili Arsenal kudondosha alama mbili muhimu siku ya jumatano dhidi ya Crystal Place timu hizo zikiisha sare ya magoli 2-2 uwanjani Emirates na kudidimiza matumaini yake ya kutwaa ubingwa wa Epl msimu huu.
Beki Jacob Kiwior aliweka uongozini The Gunners kunako dakika 3 kabla ya Palace kusawazisha kupitia kwa kiungo mshmabulizi Eze Oberechi kunako dakika ya 22 na licha ya kuchukua uongozi mwingine kupitia Leandro Trossard dakika ya 46,kilabu ya Palace ilijibu dakika ya 84 kupitia kwa mshambulizi Jean Philip Mateta.
Matokeo haya yanawacha Liverpool nafasi ya kwanza na alama 79 nayo Arsenal nafasi ya pili na alama 67 nayo mancity wakiwa nafasi ya tatu na alama 61 nayo Nottingham Forest ni ya nne na alama 60 mkiani ni vilabu vya Ipwisch Town,Leicester city na Southampton mtawalia.
News
Matokeo Yataanza Kuja Tu

Mkufunzi wa kilabu ya kiifi united Samson Jumbe amesema kwamba ana Imani vijana wake watarejea katika hali ya kupata matokeo chanya licha ya vijana wake kupoteza mechi 2 mfululizo ikiwemo debi kati yao na kilabu ya United Brothers mwishoni mwa jumwa
Kwa mujibu wa mwalimu huyo kwa sasa wanalenga kuimarisha safu yao ya mashambulizi ambayo imekua ikipoteza nafasi nyingi za wazi.
“Naamini kwa uwezo wa mwenyezi Mungu vijana wangu wataanza kufunga magoli na kuanza kushinda mechi za ligi ya kaunti kuanzia wikendi hii nyumbani,mechi ya tumecheza vizuri kasoro magoli tu.”
Kwa upande wake kocha wa kilabu ya united Brothers Titus Kitaka amesema kwamba mazoezi mazito ambayo amekua na vijana wake imewasaidia pakubwa kupata matokeo mazuri tangu ligi hiyo kungoa nanga.
“Sisi ni ushindi tu kwa sababu tufanye mazoezi ya kutosha kwa ajili ya ligi hii ya kaunti na malengo yetu yanasalia pale pale kushinda na kupanda msimu ujao.”
Kilifi United inaketi nafasi ya 9 na imepoteza mechi mbili mfululizo kati nne ambazo wamecheza huku United Brothers wakishinda tatu na kupoteza moja pekee.