Connect with us

Entertainment

Diamond Amshtaki Ex Wake Kwa Kutumia Picha Za Zamani Kum’blackmail

Published

on

Mmiliki na mjasiriamali wa lebo ya Wasafi Media na WCB Wasafi, Diamond Platnumz ameelekea mahakamani kumshtaki mpenzi wake wa zamani kwa kile alisema kwamba anatumia picha za zamani wakiwa pamoja kumchafulia jina.

Akithibitisha hatua hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond alisema kwamba mwanamke huyo ambaye hakuweka wazi utambulisho wake amekuwa akimchafulia jina kwa kutumia video za zamani wakiwa pamoja.

Msanii huyo alithibitisha kwamba ameona baadhi ya video hizo zikisambazwa na mpenzi wake wa zamani mitandaoni kwa lengo la kumharibia jina licha ya kuachana muda mrefu uliopita.

“Nimeona kuna clip zinasambazwa mtandaoni zinazonihusu…clip hizo ni za zamani, mwaka 2023, na zina zaidi ya miaka miwili nyuma…na mwanamke huyo pia niliachana nae takriban miaka miwili sasa,” Diamond alisema.

Msanii huyo alieleza kwamba video hizo zinalenga kumharibia hata penzi lake la sasa na Zuchu, akiweka wazi kwamba alishamjulisha mpenzi wa sasa kuhusu kumalizika kwa penzi hilo la zamani.

“Lakini pia nilimueleza mwenzangu niliye nae na tukasameheana na kuanza maisha mapya…” alisema.

Baada ya kugundua kwamba lengo la mwanamke huyo kutumia video hizo za zamani wakiwa pamoja ni kumharibia, Diamond alisema tayari amelikabidhi mikononi mwa idara husika kisheria.

“Mwanamke huyo sasa ameamua kutumia clip hizo na kuambatanisha na jumbe za uongo kwa lengo la kuni blackmail na kutengeneza fedha, jambo hili lishafikishwa katika mamlaka husika na taratibu za kisheria zinafuatwa. Shukran,” alisema.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Entertainment

Chameleone Aongelea Madai Kuhusu Kufungwa Gerezani, Afichua Anafanyiwa Upasuaji

Published

on

Msanii maarufu wa Uganda, Jose Chameleone, amekanusha vikali uvumi unaodai kuwa amefungwa gerezani, akibainisha kuwa yuko hospitalini kwa ajili ya upasuaji muhimu.

Haya yanajiri baada ya video ya mwanadada akidai kwamba msanii huyo amefungwa gerezani kusambazwa mitandaoni.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumanne jioni, Chameleone, ambaye jina lake halisi ni Joseph Mayanja, aliwashukuru mashabiki wake kwa upendo na maombi yao wakati wa kipindi kigumu anachopitia.

Pia alieleza kusikitishwa na video inayosambaa ikidai kuwa amefungwa, akisema:

“Ninawashukuru nyote kwa upendo na maombi yenu. Nimeona video ya mwanadada mmoja mdogo akisema uongo kuhusu mimi kuwa jela n.k. Watu wa aina hiyo wana mawazo gani, hata hivyo? Niko hapa kwa ajili ya upasuaji wangu na nitawajulisha maendeleo yangu. Asanteni watu wangu,” Chameleone alisema.

Aliambatanisha ujumbe wake na video iliyomuonyesha akiongea huku akiwa amelala katika kitanda cha hospitali.

Chameleone amekuwa akipambana na matatizo ya kiafya kwa muda.

Mwezi Desemba 2024, alilazwa katika Hospitali ya Nakasero jijini Kampala kwa siku 11 kutokana na matatizo ya kongosho.

Baadaye, alisafirishwa kwenda Hospitali ya Allina Health Mercy nchini Marekani kwa matibabu zaidi, safari iliyogharamiwa na serikali ya Uganda chini ya Rais Yoweri Museveni.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa baba yake, Gerald Mayanja, Chameleone alizidiwa na kukimbizwa hospitalini Massachusetts baada ya kuzimia asubuhi ya Jumanne, Februari 18, 2025.

Rafiki yake, Juliet Zawedde, alithibitisha kuwa msanii huyo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mapafu na kongosho.

Zawedde aliandika kwenye mitandao ya kijamii: “Rafiki yangu kipenzi hajisikii vizuri leo. Amepelekwa hospitalini. Naomba kwa ajili yako, rafiki yangu mpendwa Chameleone. Najua kwa sasa hujisikii vizuri. Bwana akupe mguso wa uponyaji, arejeshe afya na nguvu zako, akufariji katika maumivu yako, na akupe ujasiri wa kukabiliana na changamoto hii.”

Familia na mashabiki wa Chameleone wanaendelea kumuombea apate nafuu haraka. Baba yake alieleza: “Chameleone alipaswa kufanyiwa upasuaji mapema, lakini uliahirishwa ili madaktari wafanye vipimo kuhakikisha mwili wake uko tayari kwa upasuaji. Walichunguza moyo wake, shinikizo la damu, macho, na aina ya damu kabla ya kuendelea, kama taratibu zinavyotaka.”

Kwa sasa, mashabiki na wapendwa wa Chameleone wanasubiri taarifa zaidi kuhusu maendeleo yake, wakitumaini atapona na kurejea kwenye jukwaa la muziki hivi karibuni.

Continue Reading

Trending

Copyright © 2024 Coco Media.