Connect with us

News

Wazazi na Walimu wahimiza Wanafunzi kujiunga na Skauti.

Published

on

Wazazi na walimu kaunti ya Kwale wameshinikiza kuhimiza wanafunzi kujiunga zaidi na kundi la maskauti kutokana na idadi ndogo ya maskauti kaunti hiyo.

Akizungumza wakati wa kongamano la maskauti la ngazi za kaunti linalofanyika katika shule ya msingi ya Kinango kaunti ya Kwale, Kamanda wa skauti wa gatuzi dogo hilo Mambo Tsuma alieleza kuwa changamoto hiyo ya idadi ndogo inaendelea kuhatarisha uwepo wa skauti.

Baadhi ya wanafunzi maskauti kaunti ya Kwale

Kwa upande wake Mwalimu Abbas Kanyalo,aliitaka idara ya elimu ikishirikiana na viongozi wengine kukumbatia swala la skauti katika shule zote nchini na kuipa skauti kipau mbele.

Kongamano hilo la siku 3 lilijuisha shule 58 kutoka eneo hilo la Kwale ikiwemo shule za sekondari, sekondari msingi, shule za msingi na shule za wanafunzi wenye uwezo maalum.

Taarifa ya Mwanahabari.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Godhana, awataka wakaazi kutoingiza siasa miradi ya maendeleo

Published

on

By

Gavana wa kaunti ya Tana River Dhadho Godhana amewataka wenyeji wa kaunti hiyo kujiepusha na wanasiasa ambao wanaingiza siasa kwenye masuala ya maendeleo.

Godhana alisema hilo limechangia kaunti ya Tana River kusalia nyuma kimaendeleo hali ambayo itasababisha miradi mingi kuzidi kukwama.

Godhana alisema ni lazima viongozi na wenyeji wa kaunti ya Tana River washirikiane na uongozi wa kaunti ili kuafikia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Wakati huo huo Godhana aliesema mradi wa Village Cluster ambao umekuwa ukipingwa ndio utakaosaidia kudhibiti changamoto ambazo zinaikumba kaunti ya Tana River.

Naye Mahat Ali Loka ambaye ni Naibu Gavana wa kaunti ya Tana River, aliwaonya wanasiasa kutoka kaunti zingine dhidi ya kuingilia siasa za kaunti hiyo huku Spika wa bunge la kaunti hiyo Osman Noor Galole, akitoa onyo kwa wafanyikazi wa umma dhidi ya kujumu la serikali ya kaunti ya Tana River.

Taarifa ya Janet Mumbi

Continue Reading

News

Mwili wapatikana baharini Shelly Beach Likoni

Published

on

By

Polisi kaunti ya Mombasa wanachunguza kisa ambapo mwili wa mwanamme ambaye hajafahamika umepatikana ukielea katika maji ya bahari hindi kwenye ufuo wa Shelly Beach eneo bunge la Likoni.

Ripoti ya polisi ilibaini kuwa mwili huo uligunduliwa na wavuvi eneo hilo, ambao walipiga ripoti katika kituo cha polisi cha Shelly Beach kuhusiana na tukio hilo.

Polisi walisema hawakubaini mara moja anakotoka mtu huyo.

Vile vile haikubainika iwapo marehemu alizama au aliuawa kabla ya mwili wake kutupwa baharini.

Polisi walisema hawajakutana na stakabadhi zozote za kumtambulisha mtu huyo huku wakiwasihi wananchi kutoa taarifa iwapo wanafahamu familia ya marehemu.

Mwili unahifadhiwa katika hifadhi ya maiti katika hospitali ya Rufaa ya Coast General Mombasa wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading

Trending