Connect with us

Health

Vilabu Vya Burudani Kufungwa Malindi Kisa Mziki wa Sauti ya Juu

Published

on

Photo: Courtesy

Idara ya mazingira katika kaunti ya Kilifi imeanzisha mchakato wa kuvifunga vilabu na maeneo ya burudani mjini Malindi ambayo yamekuwa na tabia ya kuchezesha mziki wa sauti ya juu nyakati za usiku.

Akizungumza na Wanahabari mjini Malindi, Afisa mkuu wa idara ya mazingira kaunti ya Kilifi Zamzam Ali amesema vilabu hivyo vya burudani vimekuwa vikikiuka sheria za Mazingira hasa maeneo yalio karibu na vituo vya afya na shule.

Ali amedokeza kwamba hatua hiyo itakuwa funzo kwa watu na maeneo mengine kaunti ya Kilifi ambayo yamekuwa na tabia ya kutatiza wananchi kwa uharibifu wa Mazingira.

Kwa upande wao wamiliki wa mahoteli mjini Malindi wakiongozwa na Nicholus Ranford wameelezea kutoridhishwa na uharibifu wa mazingira huku wakiitaja tabia ya vilabu vya burudani kucheza mziki kwa sauti ya juu hasa nyakati za usiku ni kero kwa watalii.

Haya yamejiri baada ya baadhi ya vilabu vya burudani mjini Malindi kaunti ya Kilifi kuonekana kukiuka sheria za mazingira kwa kuendeleza sherehe zao kwa kucheza mziki kwa sauti ya juu.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Health

Wauguzi kaunti ya Kilifi wasitisha mgomo wao

Published

on

By

Huduma za matibabu katika hospitali na zahanati za umma kaunti ya Kilifi zimerejea kama kawaida baada ya wauguzi waliokuwa katika mgomo kusitisha mgomo wao rasmi.

Hii ni baada ya kikao cha siku nzima kati ya serikali ya kaunti ya Kilifi ikiongozwa na Gavana Gedion Mung’aro na viongozi wa Muungano wa wauguzi kaunti ya Kilifi wakiongozwa na Katibu mkuu wa Muungano huo wa wauguzi Derrick Abdallah ambapo waliafikia kutekelezwa kwa mkataba wa makubaliano wa malipo CBA.

Akizungumza na Wanahabari baada ya kikao hicho cha maafikiano, Gavana Mung’aro alisema masuala yote yalioibuliwa na wauguzi hao yatatelezwa kwa kuambatana na sheria sawa na kubuniwa kwa jopo maalum litakaloogozwa na Waziri wa Afya kaunti ya Kilifi Peter Mwarogo kutatua masuala yaliyosalia.

“Tumekuwa na kikao cha siku nzima na wauguzi wa Kilifi na mnajua kwamba walikuwa kwa mgomo wa kitaifa lakini kama kaunti ya Kilifi tumekubaliana kutekeleza masuala kadhaa waliyokuwa nayo ili kurejea kwa huduma za afya katika mkataba wa CBA na tumesema tutabuni kamati kati ya bodi ya huduma za umma na Waziri wa afya Peter Mwarogo na wauguzi kutatua masuala yaliyosalia”, alisema Gavana Mung’aro.

Gavana Mung’aro aliweka wazi kwamba barua zilizoandikwa kwa wauguzi 21 zimefutiliwa mbali, akisema watapewa barua zingine za kurejea kazini huku akionya kwamba ni lazima wauguzi kuzingatia sheria na nidhamu.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa Muungano wa wauguzi hao kaunti ya Kilifi Derrick Abdallah aliwaagiza wauguzi wote waliokuwa katika mgomo kurejea kazini katika mda wa masaa 24, akisema masuala yote ibuka ikiwemo mishahara yatatauliwa.

“Tunawahimiza wauguzi kurejea kazini katika muda wa saa 24, zile barua zilizotumwa kwa wauguzi tumeelewa zitafutiliwa mbali na leo gavana ameahidi kuongeza shilingi elfu tano katika mwaka wa kifedha wa 2024/2025 ya sare za kazi na masuala mengine muhimu pia tumeafikiana.”, alisema Derrick.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Continue Reading

Health

Eneo la Rabia linaongoza kwa idadi ya watoto ambao hawajapokea chanjo

Published

on

By

Eneo la Rabai kaunti ya Kilifi ndio eneo linaloongoza katika kaunti nzima ya Kilifi na idadi kubwa ya watoto ambao hawajapokea chanjo yoyote inayochanjwa watoto.

Haya ni kwa mujibu ya takwimu za afya kutoka kwa idara inayoshughulikiwa masuala ya chanjo katika kaunti ya Kilifi.

Muuguzi msimamizi wa masuala ya chanjo katika kaunti ya Kilifi, Christine Mataza alisema kufikia mwezi wa saba ni asilimia 36 pekee ya watoto wote kaunti ya Kilifi ambao walipokea chanjo.

Christine alisema kuwa kupitia warsha hiyo na wadau mbalimbali wakijumuisha viongozi wa kidini, mashirika na viongozi wa kijamii wamekubaliana kuimarisha hamasa mashinani kuhusiana na umuhimu wa wazazi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo

Muuguzi msimamizi wa masuala ya chanjo katika kaunti ya Kilifi, Christine Mataza

Aidha aliwahimiza wakaazi wa Kilifi kuzingatia hamasa hizo zitakazowafikia kupitia wadau mbalimbali ili watoto wao wapate chanjo akieleza kuwa ukiukaji wa baadhi ya chanjo huenda ukamsababishia mtoto ulemavu wa kudumu

Kwa upande wake msimamizi wa afya ya jamii kaunti ya Kilifi, Amos Ndenge aliitaja mikakati ambayo wameweka kuhakikisha kuwa wanafikia malengo yaliyowekwa kufungamana na idadi ya chanjo.

Viongozi wa kidini waliohudhuria warsha hiyo waliahidi kushirikiana ili kuafikia malengo ya idara hiyo ya chanjo.

Taarifa ya Hamis Kombe

Continue Reading

Trending