Sports
Tukitolewa Makundi Tutakua Tumefeli Kocha Jaribuni Sec

Mkufunzi wa Shule Ya Upili ya Jaribuni Hassan Pande amesema kwmaba iwapo watabanduliwa kwenye hatua ya makundi mashindano ya Shule za Upili ukanda wa Pwani Mpeketoni Lamu Julai 2.
Akizungumza ndaani ya Kipenga Cha Coco FM mwalimu huyo amekiri kutokana na malengo ambayo wameweka msimu huu kutoka kwenye awamu ya makundi au hata nusu fainali kama shule watakua wamefeli kwani lengo lao ni kuwakilisha ukanda huu Kitaifa mwaka huu.
“Sisi si ati kutolewa Makundi ata tukitolewa Semis tutakua tumefeli mno,tumeweka investment kubwa katika timu yetu na mwalimu mkuu amewaweka vijana sawa sawa letu ni kupata matokeo mazuri na kufuzu kitaifa.”
Kuhusu mchezo wao kuelekea mashindano hayo katika kaunti ya Lamu mwalimu huyo ameongezea kuwa mashabiki watarajie Jaribuni Tofauti na ilivyokua katika mashindano ya Kaunti.
“Mechi za Regionals najua si kama za kaunti High Intensity,kasi nyingi na mpira mwingi kwa hivyo mashabiki watarajie Jaribuni mpya kabisaa kuelekea Lamu.”
Jaribuni wamejumuisha Kundi B pamoja na : Mokowe,Serani na Tana.
Mashindano hayo yanaanza Julai 2 hadi Jula 4 Mpeketoni Lamu.
Sports
Manchester United Ndiyo mabingwa wa ‘PREMIERE LEAGUE SUMMER SERIES’

Sports
Stars yaanza vema CHAN kwa ushindi goli 1-0 dhidi ya DR-Congo
