Connect with us

News

Serikali na Wadau wa mazingira wapanda miti, Sabaki

Published

on

Serikali ya kitaifa kwa ushirikiano na mashirika ya kimazingira kaunti ya Kilifi inaendeleza mpango wa upanzi wa miti ili kuboresha mazingira.

Kulingana na Katibu wa masuala ya vijana na uchumi bunifu nchini Fikirini Jacobs, mpango huo unalenga kurudisha hadhi ya taifa la Kenya katika viwango vya kimazingira.

Akihutubia Wananchi wakati wa zoezi la upanzi wa mikoko katika eneo la Sabaki kaunti ya Kilifi, Fikirini alibainisha kwamba kupitia zoezi hilo jumla ya Miche elfu mbili ya mikoko kutoka kwa serikali na mashirika ya uhifadhi wa Mazingira imepandwa katika eneo hilo.

“Tumepanga miti mingi sana, idara yetu ya vijana imetoa miche elfu na kupitia mashirika mengi hapa wametoa miche elfu kwa jumla tumepanda miti elfu mbili, asante sana kwani kwa kufanya hivyo unasaidia pakubwa”, alisema Fikirini.

Wakati huo huo ameihimiza wananchi kuzingatia suala la upanzi wa miti pamoja na kujiepusha na ukataji miti kiholela, akisisitiza haja ya wakaazi kulinda misitu ili kuiwezesha jamii kuwa mazingira bora.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

International News

Iran Yafanya Mashambulizi Qatar

Published

on

Katika juhudi za kulipiza Mashambulio ya jeshi la Marekani dhidi ya vituo vya Nuklia, Iran Leo Jumatatu Juni 23, imevurumisha makombora na kushambulia kambi ya jeshi la Marekani likuyoko Qatar, Milki za Kiarabu.

Mashambulio hayo ya hivi Punde kabisa katika Mzozo huo wa Mashariki ya Kati, yanazidi wasi wasi katika eneo hilo la Ghuba.
Muda mfupi baada ya shambulio hilo, Bahrain na pia Qatar ambazo ni makao ya kambi ya kikosi Cha 5th Fleet Cha Jeshi la Marekani , zilisitisha mara Moja safari zote za ndege katika anga zao.

Makombora hayo ya Iran yalilenga kambi ya kijeshi ya Al Udeid, nchini Qatar, ingawa jeshi la Marekani liliweza kuyategua makombora hayo kabla ya kusababisha maafa makubwa.
Hakuna habari zozote za majeruhi zilizotolewa kufikia sasa.

Shirika la Habari la AP limeripoti Kwamba, Iran imetoa taarifa kudai kwamba makombora yaliyovurumishwa yanauzani sawa na yale yaliyotumiwa na Jeshi la Marekani kuharibu vituo vyake vya Nuklia huko Fordow.

Hata hiyo lakini, Iran inasema Kwamba ililenga kambi hiyo la Al Ufeid ambayo Iko mbali kidogo na makaazi ya Watu.
Aidha makombora hayo pia yalilenga kambi ya makaazi ya jeshi la Marekani la Ain Al-Assad iliyoko eneo la magharibi mwa Iraq.
Kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alionya kwamba, Mashambulio hayo ya Marekani yatakuwa na athari kubwa za kiusalama sio tu kwa America bali pia eneo la Mashariki ya Kati.

Mapema Leo Isreal pia ilizidisha Mashambulio yake dhidi ya Iran kulenga gereza ambalo yaaminika limekuwa likitumiwa kuwafungia wanaharakati wa kisiasa nchini humo.

Continue Reading

News

Kindiki, ataka makubaliano kati ya serikali kuu na kaunti kutekelezwa

Published

on

By

Naibu wa rais Prof. Kithure Kindiki ametaka makubaliano yote kati ya serikali za kaunti na ile ya kitaifa kutekelezwa kabla ya mwezi Disemba mwaka huu wa 2025.

Akizungumza katika makao yake ya Karen jijini Nairobi Jumatatu 23, Juni 2025, kwenye mkutano wa 27 kati ya serikali kuu na zile za kaunti kuhusu bajeti IBEC, Kindiki alisema kumekuwa na makubaliano ambayo yamekuwa hayafuatiliwi ili kutekelezwa.

Kindiki alisema serikali kuu imejitolea kuhakikisha serikali za kaunti zinafanikisha miradi mbalimbali na kuwataka maafisa wa serikali za kaunti na ile ya kitaifa kushirikiana kwa majadiliano.

Wakati huo huo alisisitiza haja ya kutafuta suluhu la matatizo yanayoathiri utendakazi wa serikali za kaunti huku akipuzilia mbali uwepo wa mzozo wowote baina ya serikali kuu na zile za kaunti.

Taarifa ya Janet Mumbi.

Continue Reading

Trending