Connect with us

News

Mashahidi zaidi wajitokeza dhidi ya Mackenzie

Published

on

Kesi dhidi ya mhubiri tata Paul Mackenzie na washukiwa wenzake 38 kuhusu ukatili na ukiukaji wa haki za watoto inaendelea kusikizwa katika mahakama ya watoto ya Tononoka, Mombasa mbele ya hakimu mkuu Nelly Chepchirchir.

Shahidi wa 43, Sajenti mwandamizi Joseph Yator, alieleza jinsi mtoto aliyenusurika kutoka Shakahola alivyoripoti kuwa watoto wawili walifunikwa nyuso na mama zao hadi kufariki baada ya kushindwa kufa kwa kufunga.

Yator alisema alipewa amri ya mahakama kufukua miili hiyo ili kubaini chanzo cha vifo hivyo, lakini baada ya Mackenzie kuachiliwa kwa dhamana ya polisi, alikuta makaburi hayo yakiwa matupu.

Aliongeza kuwa mwili mmoja kati ya hiyo miwili ulipatikana kwenye  kaburi tofauti na kupelekwa kwa vipimo vya DNA, ambapo matokeo yalionyesha kufanana kwa asilimia 99 na ndugu wa familia hiyo.

Shahidi wa 44, Julius Kiprotich, alisimulia jinsi mkewe, Alice Kawira, aliyefuata mafundisho ya Mackenzie, alivyochoma vitabu na sare za shule za watoto wao, na pia kumtoa mamake hospitalini na kutupa dawa zake, akidai matibabu ni ushetani.

Kiprotich alitoa ushahidi wa kusikitisha akieleza jinsi mkeke na wafuasi wengine wa kanisa la Good News International walivyosherehekea kifo cha mtoto wao wa pili badala ya kuomboleza, baada ya mkewe kushindwa kumpeleka mtoto hospitalini.

Alieleza mahakama jinsi mkewe alivyomtoa mtoto kwa siri kutoka shule na kuhamia Shakahola na kisha kukatiza mawasiliano.

Mama yake Julius Kiprotich, Bi. Hellena, pia alithibitisha ushahidi  wa mwanawe kwa kueleza kuwa Alice Kawira na Julius walikuwa wanandoa na walikuwa na watoto wawili, ushahidi wake pia uliunga mkono madai ya Julius kwamba Alice Kawira alimtoa mtoto wao shuleni Eldoret na kuhamia Malindi.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Godhana, awataka wakaazi kutoingiza siasa miradi ya maendeleo

Published

on

By

Gavana wa kaunti ya Tana River Dhadho Godhana amewataka wenyeji wa kaunti hiyo kujiepusha na wanasiasa ambao wanaingiza siasa kwenye masuala ya maendeleo.

Godhana alisema hilo limechangia kaunti ya Tana River kusalia nyuma kimaendeleo hali ambayo itasababisha miradi mingi kuzidi kukwama.

Godhana alisema ni lazima viongozi na wenyeji wa kaunti ya Tana River washirikiane na uongozi wa kaunti ili kuafikia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Wakati huo huo Godhana aliesema mradi wa Village Cluster ambao umekuwa ukipingwa ndio utakaosaidia kudhibiti changamoto ambazo zinaikumba kaunti ya Tana River.

Naye Mahat Ali Loka ambaye ni Naibu Gavana wa kaunti ya Tana River, aliwaonya wanasiasa kutoka kaunti zingine dhidi ya kuingilia siasa za kaunti hiyo huku Spika wa bunge la kaunti hiyo Osman Noor Galole, akitoa onyo kwa wafanyikazi wa umma dhidi ya kujumu la serikali ya kaunti ya Tana River.

Taarifa ya Janet Mumbi

Continue Reading

News

Mwili wapatikana baharini Shelly Beach Likoni

Published

on

By

Polisi kaunti ya Mombasa wanachunguza kisa ambapo mwili wa mwanamme ambaye hajafahamika umepatikana ukielea katika maji ya bahari hindi kwenye ufuo wa Shelly Beach eneo bunge la Likoni.

Ripoti ya polisi ilibaini kuwa mwili huo uligunduliwa na wavuvi eneo hilo, ambao walipiga ripoti katika kituo cha polisi cha Shelly Beach kuhusiana na tukio hilo.

Polisi walisema hawakubaini mara moja anakotoka mtu huyo.

Vile vile haikubainika iwapo marehemu alizama au aliuawa kabla ya mwili wake kutupwa baharini.

Polisi walisema hawajakutana na stakabadhi zozote za kumtambulisha mtu huyo huku wakiwasihi wananchi kutoa taarifa iwapo wanafahamu familia ya marehemu.

Mwili unahifadhiwa katika hifadhi ya maiti katika hospitali ya Rufaa ya Coast General Mombasa wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading

Trending