Sports
Kocha Wa Stars Benni Mccarthy ataja Kikosi cha CHAN

Mkufunzi wa timu ya Taifa ya Soka Harambee Stars Benni Mccarthy amekitaja kikosi cha wachezaji 30 kuanza kambi ya mazoezi kwa makala ya CHAN Agosti 3-Agosti 30 katika mataifa ya Kenya,Uganda na Tanzania.
Magolikipa:
Faruk Shikhalo (Bandari), Sebastian Wekesa (Kariobangi Sharks), Brian Opondo (Tusker FC)
Mabeki;
Siraj Mohammed (Bandari FC), Manzur Suleiman (KCB), Pamba Swaleh (Bandari FC), Abud Omar (Kenya Police),Alphonce Omija (Gor Mahia), Sylvester Owino (Gor Mahia), Michael Kibwage (Tusker), Daniel Sakari (Kenya Police), Lewis Bandi (AFC Leopards), Kevin Okumu (KCB)
Viungo;
Brian Musa( Kenya Police), Kelly Madada (AFC Leopards), Keith Imbali (Shabana), Alpha Onyango (Gor Mahia), Mathias Isogoli (KCB), Staphod Odhiambo (Ulinzi Stars), Austine Odhiambo (Gor Mahia), Ben Stanley (Gor Mahia)
Washambulizi;
Mohammed Bajaber (Kenya Police), Boniface Muchiri (Ulinzi Stars), David Sakwa (Bandari), Emmanuel Osoro (FC Talanta), Yakeen Muteheli (Ulinzi Stars), Edward Omondi (Sofapaka), Ryan Ogam (Tusker),Moses Shummah (Kakamega Homeboyz), Beja Nyamawi (Bandari)
Stars wanafungua kampeini yao dhidi ya DR.Congo uwanjani Kasarani Agosti 3.
Sports
Makocha Saba pekee Wameshinda Taji La CHAN

CHAN COUNT DOWN 16 Days to Go
Sports
Matumaini Ya United Kupata Mbeumo Yanazidi Kudidimia

Matumaini ya kilabu ya manchester united kupata huduma za kiungo mshambulizi wa kilabu ya Brenford Bryan Mbeumo yanaonekana kufifia kila kuchao.
Haya yanajiri baada ya mazungumzo hayo kukwama kwa sasa baada ya kilabu hiyo ya London kuongeza ada ya malipo ya mchezaji huyo hadi pauni milioni 70.
Kilabu ya Manchester United haiko tayari kulipa zaidi ya pauni milioni 65 kwa mvamizi huyo raia wa Cameroon.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alifunga magoli 20 ligi ya epl msimu jana.