Sports
Kocha Wa Bafana Bafana Ataja Kikosi Cha Mwisho Cha CHAN

AFRIKA KUSINI (SOUTH AFRICA)
Sports
Msururu Wa Raga Driftwood 7s Umengoa Nanga Mombasa

Mashindano ya kitaifa ya misururu ya Raga nchini mwaka 2025 yameongoa nanga mjini Mombasa, Msururu huo wa kwanza wa Driftwood 7s inafanyika katika uwanja wa Mombasa Sports Club.
Jumla ya timu 26 zinashiriki katika makundi ya wavulana na wasichana wa chini ya umri wa miaka 18 na 15, na kundi la pamoja kwa walio chini ya miaka 13, yakionyesha kizazi kipya cha vipaji vya raga nchini Kenya.
Katika mashindano ya Divisheni ya Kwanza, mabingwa watetezi Kenya Harlequins wako Kundi A dhidi ya MMUST, KU Blak Blad, na Mwamba RFC,
Kundi B linajumuisha Kabras Sugar RFC,Catholic Monks, Nakuru RFC, na Impala RFC, kundi C linajumuisha KCB RFC, Nondescripts RFC, Daystar Falcons, na wenyeji MSC Rugby huku Kundi D litakuwa na ushindani mkali kati ya Menengai Oilers, Strathmore Leos, Stallions Rugby, na Kabarak University.
Kwa upande wa Division Two, timu 36 zinashiriki katika mashindano hayo, ambapo vigezo maalum vilitumika kugawa nafasi kwa vilabu wanachama wa KRU, timu kutoka ukanda wa pwani, zile zilizofanya vizuri awali, na zile zenye historia nzuri katika mashindano.
Makundi ya Division Two ni pamoja na AP Warriors, Kilifi Titans, Likoni, na Mean Machine ambao watacheza katika Kundi A; Embu RFC, Kaya Rugby, North Coast Stormers, na MKU Thika katika Kundi B; Homeboyz RFC, Jackals, NYS Eagles, na Makueni RFC katika Kundi C; Kisumu RFC, KCNP, NYS Spades, na Sigalagala NP katika Kundi D; huku South Coast Pirates, Vihiga Granites, Zetech Oaks, na Northern Suburbs wakicheza katika Kundi E.
Mechi ya fainali ya mashindano hayo itachezwa siku ya Jumapili mwaka huu.
Sports
Mwanamieleka Hulk Morgan Aaga Dunia Akiwa Na Umri Wa Miaka 71

Mwanamieleka maarufu nchini Marekani Hulk Hogan amefariki hapo jana akiwa na umri wa miaka 71, Madaktari walithibitisha kifo chake hapo jana huku chanzo cha kifo chake kikitajwa kuwa ni tatizo la moyo.
Majina yake kamili ni Terry Bollea akiwa ni mwanamieleka aliyetamba sana miaka za 80 na 90 kule Marekani.