Connect with us

Sports

Kilabu ya Gor Mahia Iko Tayari Kukabiliana na Simba SC kwenye Simba Day

Published

on

Nahodha wa kilabu ya Gor Mahia, Philemon Otieno, ametangaza kuwa kikosi hicho kiko tayari kwa pambano lao kubwa la maandalizi ya msimu dhidi ya miamba wa Tanzania, Simba SC.

Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu ya “Simba Day” imepangwa kuchezwa hii leo Jumatano, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, ikianza saa 1:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Licha ya mazingira ya kutisha yanayotarajiwa jijini Dar, Otieno ameonyesha kujiamini, akisema kikosi hicho kimejiandaa kikamilifu kwa changamoto hiyo.
“Tuko tayari kwa mechi kubwa, tuko tayari kupambana kwa matokeo chanya,” alisema nahodha huyo.

Miamba hao wa Ligi Kuu ya Kenya waliwasili nchini Tanzania wakiwa na kikosi cha wachezaji 25, huku wakitarajia kuunganishwa na wachezaji watano wa timu ya taifa mara baada ya mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Ushelisheli.

Otieno alisifu maandalizi hayo na kusema: “Tumefanya safari vizuri na mapokezi yamekuwa mazuri. Mwaliko huu ni muhimu kwa kuwa Simba ni miongoni mwa timu bora zaidi katika ukanda huu na pia tukizingatia bado tuko katika maandalizi ya msimu mpya, mechi hii ni kipimo kizuri kwetu.”

Pambano hilo linatarajiwa kuwa jaribio muhimu kwa klabu zote mbili ambazo zinakamilisha maandalizi ya vikosi vyao kwa ajili ya misimu ya ndani.

Ingawa historia inatoa matumaini kwa Gor Mahia wakati walipoichapa Simba 2-0 kwenye Super Cup kule Nakuru mwaka 2018 Otieno amesisitiza kuwa malengo yao yapo kwenye mchezo wa sasa.
“Tumecheza na Simba hapo awali lakini yaliyopita si ndwele, tunalenga mechi ya kesho kwa lengo la kupata matokeo bora,” alisisitiza, akipuuza wazo lolote la kutegemea matokeo ya zamani.

Macho yote yatakuwa kwenye namna kikosi cha Gor Mahia, kinachochanganya wachezaji wenye uzoefu na wanaojaribiwa kipindi hiki cha maandalizi, kitakavyokabiliana na presha kali kutoka kwa mashabiki wa nyumbani wa Simba waliopakata uwanja.

Mechi hii inatarajiwa kuwa pambano kali la kusisimua, huku miamba hao wa Kenya wakitafuta kudhihirisha ubabe wao na kujiwekea kasi kuelekea msimu mpya, wakionesha utayari wa kushindana na bora zaidi wa ukanda huu.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Sports

Uingereza yawapa wapinzani onyo baada ya kuichapa Serbia 5-0, Haaland apiga mabao matano kwa Norway

Published

on

By

Timu ya taifa la Uingereza ilituma onyo kali kwa wapinzani wao wa Kombe la Dunia baada ya kuifumua Serbia 5-0 katika mchezo wa kufuzu siku ya Jumanne, huku Erling Haaland akifunga mabao matano na kuisaidia Norway kuendeleza rekodi ya ushindi wa asilimia 100.

Kwingineko barani Ulaya, Ureno na Ufaransa ziligeuza matokeo baada ya kuwa nyuma na kupata ushindi wa pili mfululizo katika harakati zao za kufuzu kwa michuano ya mwakani itakayofanyika Marekani, Mexico na Canada.

Ubora wa kikosi cha Thomas Tuchel ulitiwa shaka baada ya ushindi hafifu wa 2-0 dhidi ya Andorra siku ya Jumamosi huko Villa Park, lakini safari hii walitoa jibu tosha.

Uingereza ilidhibiti dakika za mwanzo mjini Belgrade na kufungua ubao dakika ya 33, wakati Harry Kane alipofunga bao lake la 74 la kimataifa kwa kichwa akimalizia kona ya Declan Rice. Wageni waliongeza bao dakika mbili baadaye, Noni Madueke akimalizia pasi nzuri ya kichwa kutoka Morgan Rogers na kumchambua kipa wa Serbia, Djordje Petrovic.

Bao la tatu lilipatikana dakika ya 52, Ezri Konsa akipiga shuti kufuatia mpira uliorudi baada ya adhabu ndogo na kufunga bao lake la kwanza la kimataifa.

Mpira mwingine wa adhabu uliopigwa na Rice ulipelekea bao la nne, Marc Guehi akiteleza na kufunga kufuatia faulo iliyofanywa dhidi ya Kane na Nikola Milenkovic, ambaye alionyeshwa kadi nyekundu moja kwa moja.

Mbadala Marcus Rashford alifunga kwa mkwaju wa penalti mwishoni na kukamilisha usiku bora kwa Uingereza.

Uingereza sasa inaweza kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya nane mfululizo kwenye mchezo wao ujao wa Kundi K dhidi ya Latvia mwezi ujao.

Katika mechi nyingine ya kundi hilo, Albania ilipanda hadi nafasi ya pili baada ya kuishinda Latvia 1-0 jijini Tirana.

Continue Reading

Sports

Sare Tasa na Burkina Faso Yaahirisha Ndoto za Misri Kufuzu Kombe la Dunia

Published

on

By

Matumaini ya taifa la Misri la kufuzu Kombe la Duniabado  baada ya kutoka sare tasa ya 0-0 dhidi ya Burkina Faso kwenye mechi ya Kundi A iliyochezwa Ouagadougou, Jumanne.

Kikosi cha Hossam Hassan ambacho hakijapoteza mchezo wowote kimefikisha pointi 20 na kuongoza Kundi A kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya Burkina Faso, huku kukiwa na mechi mbili pekee zikisalia kwenye mchujo.

Kwa kuwa ni washindi wa makundi pekee wanaofuzu moja kwa moja, mabingwa wa Afrika mara saba wanahitaji alama mbili pekee kutoka kwa michezo yao miwili ya mwisho ili kujihakikishia nafasi na kufanikisha ushiriki wao wa nne kwenye Kombe la Dunia. Watakutana na Djibouti na Guinea-Bissau mwezi Oktoba.

Kocha wa Misri, Hassan, hata hivyo, alisherehekea matokeo hayo ambayo yamewasogeza hatua moja karibu na kufuzu katika mashindano makubwa ya timu 48 yatakayofanyika Amerika Kaskazini mwaka ujao.

“Ni siku kubwa kwa watu wa Misri… Ningependa kuwashukuru kila mchezaji kwa juhudi zao dhidi ya timu ngumu ambayo ina wachezaji wanaocheza Premier League, Bundesliga na Ligue 1,” alisema Hassan, mshambuliaji wa zamani wa Misri aliyewaongoza kufuzu Kombe la Dunia mwaka 1990, akizungumza na kituo cha On Sport.

“Licha ya kucheza ugenini Burkina Faso, tulicheza kwa mtindo chanya na kuunda nafasi kubwa. Wakati huohuo, tulidumisha uwiano. Tungelikuwa tumefunga goli moja au mawili kabla ya mwisho,” aliongeza.

Misri ilipata pigo mapema baada ya mshambuliaji wa Manchester City, Omar Marmoush, kulazimika kutoka nje kwa majeraha dakika ya 9.

Fursa yao bora ilikuja dakika ya 67 wakati Mohamed Salah alipompasia Osama Faisal lakini shuti lake likakataliwa kwa kuotea. Trezeguet wa Misri alikosa nafasi ya kwanza ya mchezo baada ya jaribio lake kuokolewa na kipa wa Burkina Faso, Herve Koffi.

Wenyeji hawakuwa na mashambulizi mengi, huku mshambuliaji wa Sunderland, Bertrand Traore, akiongoza juhudi zao bora.

Misri walikaribia kufunga goli la ushindi dakika za mwisho, lakini Mostafa Mohamed alipoteza nafasi mbili muhimu.

Hassan, ambaye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Misri, anatarajiwa kuwa wa kwanza kuongoza taifa hilo kufika Kombe la Dunia akiwa mchezaji na pia kocha.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 59 alisema: “Lengo langu lilikuwa kufundisha timu ya taifa ya Misri. Nimekuwa nikiota kila mara jambo hilo. Nataka kutimiza ndoto ya mashabiki na kuishi kwa imani yao (kwa kuongoza timu kufuzu Kombe la Dunia).”

Continue Reading

Trending