Sports
Kikosi Cha Handiboli Ya Ufukweni Yajinoa Tayari Kwa Kombe La Dunia

Katibu Mkuu ambaye pia ni msimamizi wa mchezo wa Handiboli ya Ufukweni (Beach Handball) ya Kitaifa Bi Carolyne Nyadiero amesema kwamba mandalizi yamekamilika kwa ajili ya safari yao ya kuelekea Tunisia wikendi hii.
Akizungumza na Kipenga cha Coco Fm Bi Nyadiero amesema kwamba malengo yao ni kumaliza wa kwanza Barani Afrika na kufuzu Olimpiki Mwaka 2026 kule Dakar Senegal.
“Nataka nishukuru Mungu pili nishukuru gavana wa kaunti hii na washikadhau ikiwemo Rais wa chama cha mchezo huu na waziri wa michezo ambao wametushika mkono tangu tulipopokea barua ya mashindano haya,Lengo letu ni kushinda ubingwa na kushiriki olimpiki 2026 nchini Senegal.
Kwa upande wake kocha wa kikosi cha wanaume Boaz Maroko amesema kwamba mandalizi ya kikosi hicho yamekua mazuri na wanalenga kushinda kombe hilo ama kuwa bora barani afrika.
“Tumejiandaa tangu mwaka jana na vijana wako katika hali shwari tunataka wa kwanza barani afrika kando na kushinda ubingwa wa kombe hili la dunia.”
Ni kauli ambayo imeweza kuungwa mkono na kocha wa kikosi cha akina dada Titus Kasekwa.
“Tumejiandaa vizuri zaidi Makala yaliyopita tulipata silver ila mwaka huu tunataka kupata tuzo kuu na kunyakua dhahabu kwenye mashindano haya.
Kikosi hicho kinakamilisha mazoezi yake siku ya Ijumaa kabila kuondoka Jumamosi kwa kombe la dunia nchini Tunisia.
Sports
Manchester United Ndiyo mabingwa wa ‘PREMIERE LEAGUE SUMMER SERIES’

Sports
Stars yaanza vema CHAN kwa ushindi goli 1-0 dhidi ya DR-Congo
