Connect with us

Entertainment

Christina Shusho Azua Gumzo Baada ya Kumsifia Rais Samia

Published

on

Msanii maarufu wa muziki wa Injili kutoka Tanzania, Christina Shusho, amezua mjadala mkali mitandaoni baada ya kumpongeza hadharani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Hatua hii imewakera baadhi ya mashabiki wake ambao walionesha wazi kutoridhishwa na ujumbe huo.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Shusho alichapisha picha rasmi ya Rais Samia, akifuatisha na maneno ya maombi:

“Neema ya Mungu ikutoshe mama, tunamtukuza Mungu kwa ajili yako.”

Aliendelea kwa kuandika:
“Fanya kwa uwezo wako wa kibinadamu, Mungu atafanya yaliyosalia. Wewe ni fahari yetu, Amina.”

Ingawa ujumbe huo ulionekana wa heshima na maombi, wengi walitafsiri kama kumsifu Rais bila kuzingatia changamoto mbalimbali za kijamii na kisiasa zinazolikabili eneo la Afrika Mashariki, hususan Tanzania na Kenya.

Sehemu ya mashabiki wake walihoji uamuzi wake wa kutoa tamko hilo, huku baadhi wakifurika kwenye sehemu ya maoni wakieleza hasira zao.
Mmoja aliandika kwa ukakasi:

“Unfollow Shusho button.”

Wengine walienda mbali zaidi na kutaka afungwe au kupuuzwa kabisa, wakidai amepuuza hali halisi ya wananchi wa kawaida.

Wachambuzi wa mitandao wanaona kuwa kundi kubwa la wafuasi wake kutoka Kenya pia walihisi kusalitiwa, hasa kwa kuzingatia muktadha wa hivi karibuni wa kisiasa na kijamii unaohusisha nchi hizo mbili.

Hali hii inaibua swali pana kuhusu nafasi ya wasanii maarufu katika kujieleza kisiasa—je, wana uhuru wa kuunga mkono viongozi bila kuhukumiwa, au wanapaswa kuwa sauti ya umma kwa kuzingatia hali halisi?

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Entertainment

Penzi Lao Lazaa Matunda: Jux na Priscilla Watarajia Mwana

Published

on

Binti wa mwigizaji mashuhuri wa Nollywood, Iyabo Ojo, ambaye ni Priscilla Ojo, na mumewe, nyota wa muziki kutoka Tanzania Juma Jux, wametangaza kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza.

Wapenzi hao walishiriki habari hizo njema kupitia mtandao wa Instagram kwa picha maridadi za ujauzito, ambapo Priscilla alionekana akionyesha tumbo lake la ujauzito. Picha hizo zilifuatana na maandishi mafupi: “Mum & Dad.”

Safari ya kimapenzi ya wawili hao imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu, ikijumuisha harusi kadhaa zilizofanyika nchini Nigeria na Tanzania, hatua ambayo iliangazia muunganiko wa tamaduni zao mbili.

Juma Jux alimvisha pete ya uchumba Priscilla mara mbili, ambapo ombi la pili lilikuwa la kipekee na lisilosahaulika, lililofanyika jijini Lagos, Nigeria.

Wapenzi hao waliadhimisha safari yao ya ndoa kwa sherehe mbalimbali, zikiwemo harusi ya kitamaduni ya Kiyoruba, harusi ya kanisani (white wedding), na sherehe nyingine zilizoandaliwa kwa fahari kubwa mnamo Aprili 17 na 19, zote zikiwa jijini Lagos.

Kadiri wanavyojiandaa kwa ujio wa mtoto wao wa kwanza, pongezi na salamu za heri kutoka kwa mashabiki na jamaa zimekuwa zikitiririka kwa wingi.

Continue Reading

Entertainment

Lisemwalo Lipo, Apewe Nafasi Afunguke, Kaa la Moto Amkingia Kifua Kelechi Africana

Published

on

Msanii nguli wa muziki Afrika Mashariki, Kaa la Moto, amekingia kifua kauli ya msanii mwenzake Kelechi Africana aliyedai kuwa “kinachowafelisha wanamuziki wa Mombasa ni ukahaba.”

Akizungumza na meza ya burudani ya Coco FM, Kaa la Moto alieleza kuwa anaamini nia ya Kelechi si ya kubeza bali ya kutaka kuona mabadiliko chanya kwenye tasnia ya muziki kutoka ukanda wa Pwani.

“Ameona ndio maana anayakemea,” alisema Kaa la Moto kwa utulivu.

“Naamini kwamba ana ufahamu sahihi, na pia naamini kuwa ni kijana ambaye anataka maendeleo ya sanaa kutoka mkoa wake. Kwa hiyo watu walipatie fikra—kwa sababu lisemwalo lipo. Labda ana kitu, akipewa nafasi atazungumza zaidi.”

Kauli ya Kelechi ilizua hisia mseto mitandaoni baada ya kupachikwa kwenye ukurasa wake wa Facebook, ambapo aliandika: “Kinacho felisha wanamuziki wa Mombasa ni ukahaba.”

Wengine waliona ni matusi kwa jumuiya ya wasanii, lakini kwa Kaa la Moto, ilikuwa ni hoja yenye mzizi wa ukweli. Alisisitiza kuwa hakuna hoja inayopaswa kupuuzwa kabla ya kueleweka kwa undani.

“Sipingi hoja yake kwa sababu kila hoja ipo huru kwa aliyeifikiria na kuiwaza. Naamini anajaribu kuinspire vijana wenzake,” aliongeza Kelechi.

Katika mazungumzo hayo, Kaa la Moto pia alitumia fursa hiyo kueleza kinachomuweka relevant kwenye muziki licha ya mabadiliko ya ladha, mitindo, na majina mapya kwenye game kila mwaka.

“Kitu ambacho kimeniweka hadi leo ni nidhamu. Nidhamu kwenye maisha, kwenye kazi, kwenye watu,” alisema kwa msisitizo.

Baadhi ya mashabiki waliopena maoni yao kwenye post ya Kelechi walisema;

Tamara Black, “Shida tu unaingililia watu hawana shughuli yako.Put that effort in Use ututolee kazi kali umbea achia watoto wa kike.”

Raisi Wakitaa, “Apo umenena nimepata mwenzangu sasa wakusema ukweli wanaboesha Sana Kwanza uyo my wife ndo kabisa simuelewi kila siku post ya mtu mmoja demu mwenyewe alishaliwa na wahuni toka enzi za shule 😁.”

D Jay Ricious,”Wapashe adi wagutuke maana tulio chini ni huko juu ndio twaja kwa nafasi zetu. #coast music occupy kenya 🇰🇪.”

Hamza Ahmed Lama, “Acha kutafuta Kiki’kai anapiga hela na anamadili kibao.”

Knasty Snaty, “Wew nawew wataka dera kazi yako ni umbea tu acha mziki uanze umbea.”

Continue Reading

Trending