Connect with us

Entertainment

#CHAN2024: Savara, Zuchu na Eddy Kenzo Kutumbuiza Fainali ya CHAN 2024 Nairobi

Published

on

Mashindano ya CHAN 2024 yakielekea ukingoni, mashabiki wanatarajiwa kupata burudani ya aina yake kutoka kwa baadhi ya nyota wakubwa wa muziki Afrika Mashariki.

Kenya, Uganda na Tanzania zitawakilishwa vilivyo kupitia majina makubwa matatu: Savara wa Kenya (mwanachama wa zamani wa kundi maarufu Sauti Sol), Eddy Kenzo wa Uganda, na Zuchu kutoka Tanzania, anayejulikana kwa jina halisi Zuhura Othman.

Onyesho hili la kufunga pazia litafanyika sambamba na mechi ya fainali Jumamosi, likitarajiwa kuhamasisha na kuburudisha maelfu ya mashabiki watakaofurika uwanja wa Kasarani. Shoo hiyo inalenga kumaliza mashindano haya ya kihistoria kwa upekee na kiwango cha juu cha burudani.

Mbali na kusubiriwa kwa hamu jukwaani, Savara pia amekuwa na mchango mkubwa nyuma ya pazia. Yeye ndiye mtunzi na mtayarishaji wa wimbo rasmi wa CHAN 2024 unaoitwa “Pamoja”.

Wimbo huo unashirikisha nyota kutoka kanda hii: Elijah Kitaka wa Uganda na Phina wa Tanzania. Uliimbwa kwa mara ya kwanza katika sherehe za ufunguzi na uliweka ladha na hamasa ya mashindano haya.

Ingawa wenyeji wa mashindano haya—Kenya, Uganda na Tanzania—waliishia katika hatua ya robo fainali, fainali za mwaka huu zinaahidi kuwa kilele cha msisimko.

Burudani kutoka kwa Zuchu, Savara na Eddy Kenzo itakuwa chachu ya kuhitimisha mashindano yaliyojaa matukio na hisia.

Kwa upande mwingine, kumekuwa na malumbano mitandaoni kati ya mashabiki wa Kenya na Tanzania, hususan baada ya timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, kudondoshwa nje ya michuano hiyo katika robo fainali.

Mashabiki wa Tanzania hawakusita kuchokoza wenzao kwa kejeli, jambo lililoongeza ladha ya ushindani wa nje ya uwanja.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Entertainment

Mboga Imejileta; Arrow Bwoy Aitisha Pigano Dhidi ya Shakib

Published

on

Msanii maarufu wa Kenya, Arrow Bwoy, amezua gumzo mtandaoni baada ya kumualika wazi wazi mfanyabiashara kutoka Uganda, Shakib Cham, kwenye pambano la ndondi.

Hii imekuja baada ya kipigo cha hadharani ambacho Shakib alipokea kutoka kwa msanii mwenzake wa Uganda, Rickman, hali iliyoacha mashabiki wengi wakisema: “Sasa ata Arrow Bwoy anaweza!”

Kupitia video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Arrow Bwoy, anayefahamika kwa vibao kama Digi Digi, hakuonyesha woga wowote. Kwa ucheshi, alisema amekuwa akisubiri nafasi kama hii kwa muda mrefu.

“Mboga imejileta,” alisema kwa kujiamini, akimaanisha kuwa Shakib amejileta mwenyewe kwenye kipigo.

“Chakula kiko tayari. Niko tayari kwa pambano hili.”

Arrow Bwoy pia hakusita kumtaja mke wa Shakib, Zari Hassan, akimtaka akae mbali na ulingo siku ya pambano hilo kwa usalama wake binafsi.

“Zari, usijisumbue kuja. Hii si sehemu ya wanawake. Usije ukazimia tukapata janga la pili,” alisema kwa kejeli.

Hata hivyo, wakosoaji wake walikumbusha jamii kuhusu video za awali zinazoonyesha Arrow Bwoy akichapwa na polisi wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha. Swali likabaki: Je, kweli ana uwezo wa kumpiga Shakib au ni porojo za mitandaoni?

Kwa jina la Zari kuingizwa kwenye sakata hili, mvutano umeongezeka na mashabiki kote Afrika Mashariki wanasubiri kuona kama Shakib atakubali changamoto hii ya kihistoria.

“Zari, kama unasikia, mtume tu kijana wako aje achukue kichapo — kichapo cha kimataifa,” Arrow Bwoy alimalizia kwa msisitizo.

Kwa sasa, macho yote yako kwa Shakib. Je, atakubali changamoto hii na kuweka historia mpya ya burudani Afrika Mashariki?

Continue Reading

Entertainment

Zuchu Kutumbuiza Kwenye Mechi ya Fainali ya CHAN 2024

Published

on

Msanii nguli kutoka Tanzania, Zuchu, anatarajiwa kutumbuiza kwenye mechi ya Fainali ya CHAN 2024 Jumamosi, Agosti 30, 2025 jijini Nairobi.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Zuchu alieleza furaha yake kwa nafasi hiyo kubwa akisema:

“Ninafuraha kubwa kutangaza kuwa nitakuwa ndiye msanii mkuu kwenye fainali za mashindano ya CHAN….”

Fainali hiyo inakutanisha Morocco na Madagascar ambayo iliitoa Kenya kwenye hatua ya robo fafainali.

Ikumbukwe kuwa wandaaji wa michuano hii Kenya, Uganda na Tanzania walitolewa nje ya michuano hiyo katika hatua ya robo fainali.

Kenya ilitolewa na Madagascar kupitia mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare ya goli moja kwa moja huku Tanzania ikifungwa goli moja na Morocco.

Senagal waliifunga Uganda goli moja katika dakika ya 62 ya mchezo.

Mashindano ya CHAN yanayoshirikisha timu za taifa za wachezaji wanaocheza ligi za ndani, yamekuwa jukwaa kubwa la kuonyesha vipaji vipya vya soka barani Afrika.

Mwaka huu, mbali na kivutio cha uwanjani, shoo ya Zuzhu itazidisha hamasa na kuleta burudani ya kipekee kwa mashabiki watakaofurika Uwanja wa Kasarani.

Zuzhu, ambaye amejizolea mashabiki kutokana na muziki wake wenye ladha ya kipekee na ujumbe unaogusa mioyo, anazidi kuthibitisha nafasi yake kama msanii anayevuka boda.

Onyesho hili litakuwa ishara nyingine ya jinsi muziki wa Afrika Mashariki unavyopata nafasi kubwa kwenye matukio ya kimataifa.

Continue Reading

Trending