Connect with us

News

Bunge la kaunti ya Kilifi linarejelea vikao vyake Rasmi

Published

on

Bunge la kaunti ya Kilifi linarejelea vikao vyake Agosti 4, 2025 baada ya kuahirishwa kwa mda wa majuma mawili.

Hii ni baada ya bunge hilo mnamo Julai 21, 2025 kuandaa kikao maalumu cha kupiga kura ya kujaza nafasi ya spika wa bunge hilo, iliyowachwa wazi baada ya wawakilishi wadi kumbandua mamlakani Teddy Mwambire Juni 30, 2025.

Katika uchaguzi huo Catherine Kenga aliibuka mshindi kwa kuapata kura 41 dhidi ya 51 na kuwashinda wapinzani wake wengine 4.

Mwishoni mwa wiki jana Kenga alitangazwa rasmi kupitia gazeti la serikali kama spika wa bunge la kaunti ya Kilifi na kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhfa huo katika kaunti hiyo.

Majukumu ya kwanza kwa Spika huyo ni kuunganisha bunge hilo ambalo limeonekana kugawanyika kufuatia hoja iliyowasilishwa na kiongozi wa wachache Tom Chengo wa chama cha PAA ya kumuondoa mamlakani Mwambire.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

ODM yapinga barua ya Orengo kujiuzulu

Published

on

By

Chama cha ODM kimepinga barua inayosambaa mitandaoni ikidai gavana wa kaunti ya Siaya James Orango amejiuzulu wadhifa wake.

Barua hiyo ilidaiwa kutoka kwa gavana Orengo na kuelekezwa kwa spika wa bunge la kaunti ya Siaya, pamoja na naibu gavana, baraza la magavana pamoja na kinara wa ODM Raila Odinga.

Kupitia mtandao wa X chama cha ODM kimechapisha kuwa kinauhakika barua hiyo sio sahihi na kuwataka watu kuipuuza.

Katika barua hiyo, kilichoangaziwa ni hali ya afya ya Orengo kama chanzo cha kujiuzulu, hali ambayo imedaiwa kutekelezwa kwa majadiliano na familia yake.

Barua ya kupotosha inayosambaa mtandaoni kuhusu gavana James Orengo kujiuzulu.

Orengo amekosa kuonekana hadharani kwa majuma kadhaa hali inayoibua wasiwasi miongoni mwa wakaazi anaowawakilisha.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading

News

Maabara ya siri ya dawa za kulevya yafichuliwa Kwale

Published

on

By

Idara ya usalama katika kaunti ya Kwale imefichua maabara ya siri ya dawa za kulevya katika kijiji cha Mwabungo eneo la Ukunda.

Kulingana na vyanzo vya usalama maabara hiyo iko ndani ya shamba la ekari moja lililoweza kuunganishwa na ukuta wa lango lenye ulinzi mkali.

Baada ya siku kadhaa za upelelezi wa kisiri na ukusanyaji wa taarifa za kiinteligensia, kikosi cha kitengo maalum cha kupambana na ulanguzi wa dawa za kulevya kwa ushirikiano na maafisa wa polisi kiliendesha msako wa kushtukiza eneo hilo.

Maafisa waliwakamata watu wawili mmoja akiwa raia wa Italia mwenye umri wa miaka 37, mwengine akiwa ni Moses Nanoka.

Vile vile walikamata vifaa vya maabara, kemikali zinazoshukiwa kutumika kutengeneza dawa za kulevya.

Msako zaidi ulibaini shamba hilo limetumika kupalilia bangi na kuonyesha kuwepo shughuli haramu za mda mrefu.

Washukiwa wanatarajiwa kuwasilishwa mahakamani.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading

Trending