Sports
INZAGI Bado Yuko Saana Inter.

Uongozi wa klabu ya Inter Milan uko radhi kurefusa mkataba wa kocha Simone Inzaghi licha ya kufeli
kutwaa taji la klabu bingwa Uropa siku ya jumamosi.
Rais wa Inter Giuseppe Marotta, ameelezea Imani kwa uongozi wa Kocha Inzaghi, licha ya kibano cha
magoli 5-0 klabu hiyo ilipokea katika fainali ya klabu bingwa uropa dhidi ya Paris Saint-Germain
(PSG) na kupoteza fainali ya pili mtawalia, ya kwanza ikiwa msimu wa mwaka 2022/2023 mikononi
mwa Manchester City.
Mkataba wa Inzaghi unakamilika mwezi juni mwaka ujao ila Marotta, amesisitiza kuwa mazungumzo na
kocha huyo yataanza hivi karibuni, baada ya tetesi kuwa Inzaghi anajiondoa Inter na hatakuwepo
kuitayarisha kwa ajili ya msimu ujao.
“Kushindwa katika fainali hauna msukumo wowote, inzaghi ana mkataba wa mwaka mmoja Zaidi na
tuliamua kukutana naye juma hili” Alisema Marotta katika kikao na wanahabari baada ya fainali ya klabu
bingwa uropa huko Munich Ujerumani. “Mafanikio yote na makali ya klabu yanayoonekana ni kwa ajili
ya uwezo na utaalam wake,Tutafurahia iwapo yuko radhi kuendelea na kazi.”
Sports
Ligi Limetuponyoka Asema Zico

Mkufunzi wa Kilabu ya Gor Mahia Zedekiah Zico Otieno amekubali kwamba ligi imewaponyoka baada ya kutoka sare na kilabu ya Afc Leopards ugani raila odinga katika debi la Mashemeji jana jioni.
Kiungo matata Austine Odhiambo aliweka uongozini Kogalo kipindi cha kwanza dakika ya 30 kabila ya Brian wanyama kuisawazishia chui dakika ya 55 kipindi cha pili na kocha huyo anaamini taji limewatoka baada ya sare hiyo inayowacha nafasi ya tatu.
“Tulianza Vizuri lakini concetration lapse imetucost kipindi cha pili,lengo letu lilikua kupata ushindi hapa ili kuweka pressure kwa viongozi lakini sasa matokeo haya ni ishara tosha sasa itabidi tuangazie taji la Mozzartbet Cup.”
Kwa upande wake Mkufunzi wa Afc Leopards Fred Ambani amesema kwamba ameridhishwa na matokeo hayo akijigamba angali kupoteza mechi ya Debi akiwa mchezaji na sasa kama kocha wa Ingwe.
“Vijana walioanza mechi kwa mchecheto na uoga mwingi katika kipindi cha kwanza ila tulipoenda katia dressing room nikawambia watulie na ndiposa tukarejea mchezoni,ningali kupoteza debi kama mchezaji sikuwahi na sasa kama kocha pia bado sijapoteza.
Gor inasalia ya tatu na alama 55 huku Afc Leopards wakibaki ya sita na alama 47.
Sports
Chelsea Kumtambulisha Delap

Mshambulizi wa kilabu ya Ipswich Town na timu ya taifa Uingereza Liam Delap amekamilisha sehemu ya kwanza ya vipimo vya kimatibu anapokamilisha uhamisho wake katika kilabu ya Chelsea.
Kwa mujibu wa gwiji wa uhamisho barani ulaya Fabrizio Romano uhamisho huo ni wa pauni milioni 30 Delap akitarajiwa kumwaga wino mkataba wa miaka mitano stamford bridge.
Licha ya kumulikwa na vilabu kadha wa kadha ikiwepo Manchester United pamoja na Newcastle United Delap aliamua kwamba chaguo lake ni Chelsea msimu huu na atakua sajili wa kwanza kwa kocha Enzo Maresca.
The Blues wanatarajiwa kumtambulisha hii leo mchezaji huyo ambaye alipachika wavuni magoli 12 msimu huu na kutoa pasi mbili kwa wenzake kufunga msimu ambao umekamilika.
Vijana hao wanaaminika pia kusaka mshambulizi tajika msimu huu wakimulika mshambulizi Victor Gyokeres na Victor Osimhen inaamnika pia wanamfukuzia winga wa Bilbao Nico Williams.