News
Kilabu Ya Liverpool Yamnasa Frimpong

Beki wa kilabu ya Bayern Leverkusen Jeremie Frimpong ni rasmi amejiunga na mabingwa wa ligi kuu Uingereza Liverpool.
Beki huyo mholanzi amejiunga na The Reds kwa pauni milioni 29.5 na amemwaga wino mkataba wa miaka 5 na kilabu hio kuchukua nafasi ya Alexander Trent Arnaold ambaye ni rasmi amejiunga na kilabu ya Real Madrid.
Mholanzi huyo anakua mchezaji wa tano kuvalia jezi ya kilabu hio wengine akiwa ni pamoja na Cody Gakpo,Virgil Van Dijik,Ryan Gravenberch.
Nyota huyo ambaye pia amekuwa akiwindwa na Manchester United na miamba wa Uhispania Rea Madrid amesema kwamba alichagua kilabu hiyo kwani ndio inaendana na mipango yake ya mbeleni kama mchezaji akiahidi kushinda mataji na miamba hao wa Uingereza.
News
Rais Ruto amewaongoza wakenya kuadhimisha sherehe za Madaraka za 62

Rais William Ruto amewaongoza wakenya katika kuadhimisha sherehe za Madaraka za 62 tangu taifa lijipatie uhuru.
Katika maadhimisho hayo ambayo yamefanyika katika uwanja wa Raila Odinga kaunti ya Homabay, Rais Ruto amesema taifa limepiga hatua kidemokrasia na maendeleo tangu lijipatie uhuru.
Kiongozi wa taifa ametoa changamoto kwa wakenya kuhakikisha wanaweka kipau mbele masuala ya kutekeleza mabadiliko yanayoleta ufanisi wa Taifa.
Wakenya washeherekea Madaraka, Homabay
Naye Naibu rais Prof Kithure Kindiki amemhakikishia Rais Ruto kuwa ataendelea kushirikiana naye katika kuunganisha taifa huku akimtaja Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga kama kiongozi aliyechangia zaidi mshikamano wa taifa.
Kwa upande wake Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga amemtaka Rais Ruto kuhakikisha serikali inafidia familia za wakenya walipoteza wapendwa wao wakati wa Maandamano ya vijana wa Gen Z mwezi Juni mwaka jana.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya sherehe za mwaka huu ni “uchumi wa sanawati na maswala ya bahari”, huku ikilenga kuangazia fursa za kiuchumi zinazotokana na raslimali ya maji.
News
Achani: Kaunti ya Kwale imepiga hatua katika uchumi samawati.

Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani amesema kaunti ya Kwale imepiga hatua katika kuimarisha sekta ya uvuvi na uchumi samawati.
Gavana Achani ameihimiza serikali ya kitaifa kuhakikisha inawekeza zaidi katika masuala ya uchumi samawati hasa kupitia bandari ya Shimoni, akisema itafungua ajira kwa vijana na kuboresha uchumi wa kaunti.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya sherehe za 62 za Madaraka katika eneo la Kinango, Gavana Achani amesema bandari ndogo 9 katika kaunti hiyo zimeboreshwa na vifaa vya kisasa ili kuchangia uhifadhi wa samaki.
Maadhimisho ya sherehe za Madaraka eneo la Kinango
Hata hivyo Viongozi waliohudhuria sherehe hizo katika gatuzi dogo la Kinango wakiongozwa na Mbunge wa Kinango Gonzi Rai, wamesisitiza haja ya viongozi pamoja na wananchi kumuunga mkono Rais Ruto katika kufanikisha ajenda ya maendeleo.
Kwa upande wake Kamishna wa kaunti hiyo Stephen Orinde amesisitiza umuhimu wa wakenya kuunga mkono miradi ya serikali hasa uchumi samawati na masuala ya bahari ili kupiga hatua kimaendeleo.